MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAPAA,KINABO AFAFANUA,SOMA HAPO KUJUA
Mary Kinabo -Afisa Mwandamizi wa Soko la Hisa DCE akizngumza na wanahabari Jijini Dar es salaam |
Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) katika kipindi cha
wiki iliyopita yameongeza kwa asilimia 65 kutoka Sh. Bilioni 19.6 na kufikia
bilioni 32.5.
Afisa Masoko Mwandamizi wa DSE,
Mary Kinabo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,
amesema kilichochangia mauzo hayo kupanda ni ongezeko la uhitaji wa hisa kwa
kampuni wanachama wa soko hilo na wateja wanaohitaji kununua.
Amesema idadi ya hisa
zilizouzwa na kununuliwa zimepanda zaidi ya mara nne kutoka milioni 2.4 na
kufikia milioni 9 za kitanzania.
Hata hivyo, Kinabo amesema
kutokana na kushuka kwa bei kwenye kaunta za NMB na ACA, mtaji wa soko la DSE,
umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka trilioni 21.579 hadi 21.49 trilioni.
Pia amesema mtaji wa makampuni
ya ndani umepanda kwa asilimia 0.36 kutoka trilioni 8.1 hadi trilioni 8.14.
Aidha, Kinabo amesema Sekta ya
viwanda imepanda kwa pointi 26.16, sekta ya huduma za kibenki na kifedha
imeshuka kwa alama 0.52 na sekta ya huduma za kibiashara imeshuka kwa alama
4.19.