Zinazobamba

JAJI MTUNGI ANAUAIBISHA UJAJI,MAAMUZI YAKE KWA LIPUMBA YAZIDI MWEKA MSALABANI,SOMA HAPO KUJUA



 Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

JAJI Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, ameweka pamba masikioni. Hasikii la mnadi swala wala sauti ya Kanisa. Huenda akatia doa zaidi ofisi yake iwapo CUF itambwaga mahakamani baada ya kufungua kesi dhidi yake na washirika wake, anaandika Pendo Omary.

Wakati Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam ikitoa kibali jana kwa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF), kufungua kesi ya dhidi ya Jaji Mutungi, anayetuhumiwa kuendesha shughuli za vyama vya siasa kinyume cha sheria, tayari Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF alishamuonya kwa barua siku za nyuma.

Barua ya Maalim Seif kwenda kwa msajili ambayo MwanaHALISI online imeiona, iliandikwa tarehe 4 mwezi huu, ikiwa na Kumbukumbu Na. CUF/HQ/KM/2016/21.
“Uzoefu tulioupata kupitia barua yako Kumb. Nam. HA.322/362/14/85 ya tarehe 23 Septemba, 2016 iliyokuwa na kichwa cha maneno, Msimamo na ushauri wa msajili wa vyama vya siasa kuhusu uongozi wa kitaifa wa Chama cha The Civic United Front, umetuonesha kuwa badala ya kutoa maoni, umejipa mamlaka ya Mahakama na kutoa uamuzi,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Katika sehemu nyingine ya barua hiyo, Maalim Seif  amemuonya Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba, vitendo vyake ni kinyume na Sheria ya Vyama Vya Siasa, Sura ya 258.
“Hayo unayofanya ni mamlaka ya Mahakama. Badala yake wewe unapewa mamlaka ya kuhifadhi kumbukumbu na taarifa za vyama vya siasa. Tafadhali rejea tena maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam katika Shauri la Madai Na. 6 la mwaka 2003 baina ya Emmanuel Nyenyemela na wenzake dhidi ya msajili mbele ya Jaji Thomas Mihayo.
Ukurasa wa pili wa hukumu hiyo unaeleza wazi kuwa; I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make, Inasomeka zaidi barua hiyo.
Itakumbukwa kuwa uamuzi na muongozo huo wa Mahakama Kuu uliotolewa na Jaji Mihayo haukuwahi kutenguliwa na mahakama nyingine yoyote.