Zinazobamba

WATANZANIA WAFANYIWA KITU MBAYA NCHINI KONGO,SOMA HAPO KUJUA



Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
WATANZANIA 12 jana wametekwa katika eneo la Namoyo, Jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) na kikundi cha waasi cha Maimai, anaandika Aisha Amran.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa watu hao ni madereva wa malori na kwamba, baada ya kutekwa wakiwa katika magari yao, walishushwa na kupelekwa porini na kisha malori yao manne kuteketezwa kwa moto.

Kati ya malori hayo, nane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa kitanzania, Azim Dewji na mengine ni ya wafanyabiashara kutoka Kenya.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni kwamba walipwe fedha kiasi cha Dola za kimarekani 4,000 (zaidi ya milioni Sh. Milioni 8 za Tanzania) kwa kila dereva ili waweze kuwaachia mateka hao.
“Wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha wanachokitaka itakapofika saa 10 jioni leo ingawa katika tukio hilo madereva wawili wa kitanzania, wamefanikiwa kutoroka ambao ndiyo waliosaidia kutoa taarifa rasmi,” imeeleza taarifa hiyo.
Serikali ya Tanzania imedai kuwa, tayari imechukua hatua za awali za kuwasiliana na serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa kwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama.
Hata hivyo serikali haijafafanua kuwa, ni hatua gani zimechukuliwa ili kuwaokoa madereva hao, kama ni kulipa kiasi cha fedha kinachohitajika au la.
Tukio hili ni la pili kutokea katika miaka ya hivi karibuni ambapo mwaka 2015 Mashekhe kutoka Tanzania walitekwa nchini DRC, lakini walifanikiwa kuachiwa huru bila madhara yoyote.