UVCCM NI MBUMBUMBU,CHADEMA WARUSHIA KOMBORA,SOMA HAPO KUJUA
UDHAIFU katika kutambua masuala ya kiuongozi
kunaufanya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwenda hovyo, anaandika Dany Tibason.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) ambapo
amewataka UVCCM kurudi darasani ili kujifunza masuala uongozi.
Amesema, vijana hao wanafanya siasa za kitoto
kutokana na kukosa misingi ama hekima za kiuongozi.
Katambi ametoa kauli hiyo kutokakana na tamko la
UVCCM la ‘kuwatusi’ viongozi wa dini pamoja na asasi nyingine kwa kuwataka
kutojihusisha katika mazungumzo ya kumshauri rais juu ya mwenendo wa kisiasa
nchini.
Katambi amesema, UVCCM ni watoto kwa kuwa,
wanaropoka maneno ambayo hawayajui hasa pale wanapowabeza viongozi wa dini
pamoja na taasisi mbalimbali ambazo zinatafuta usuluhishi wa kisiasa nchini.
“Vijana wa UVCCM bado ni watoto wadogo lakini pia
wanatakiwa kupelekwa shule wakasome kwanza ili waache kuropoka. Tamko lao la
juzi lilikuwa na maneno mengi ambayo yanaonesha kuwa viongozi hao ni watoto.
“Mtu mwenye akili hawezi kuhoji na kujenga mashaka
heti Chadema hawakuzungumza na viongozi wa dini na taasisi mbalimbali ili
kusitisha maandamano ya Ukuta ili kuruhusu mazungumzo kati ya viongozi wa dini
na taasisi kuzungumza na rais.
“Sasa wanataka viongozi wa dini watajwe ili iweje na
wakiwajua hao viongozi wanataka kuwafanya nini, sisi tunachokiangalia siyo
kumtaja mtu bali ni kuangalia amani inapatikana kwa njia gani,” amesema na
kuongeza;
“Siasa siyo kuropoka na kupiga kelele, siasa ni
kujenga hoja kwa mafanikio ya taifa kwa ujumla na sio ujinga kama unaofanywa na
UVCCM.”
Hata hivyo, amesema kwa sasa Watanzania wanatambu na
kujua nani kichaa, nani mkweli na ni nani ambaye anamkandamiza mwingine.
Kutokana na hali hiyo Katambi amesema, haoni sababu
ya kuendelea kuwajibu UVCCM.