SERIKALI YAPITISHA MISWAADA HII KUWA SHERIA,SOMA HAPO KUJUA
Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli ameridhia na kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili
za nchi.
Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa
Bunge la 11 leo mjini Dodoma.
Miswada iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya
Fedha na Matumizi ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria
ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya
Sheria Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi
ya Umma namba 5 ya mwaka 2016.
Aidha, Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na
kuelewa kila kinachokuja Bungeni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge
ipasavyo kwa niaba ya wananchi waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea
maendeleo.
Wabunge wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya
uwakilishi wa wananchi ili waweze kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia
haki, ustahimilivu, busara, hekima na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya
Bunge.
Vile vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt.
Tulia Akson kuongoza vema mkutano wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na
kumalizika Juni 30 mwaka huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew
Chenge, Mussa A. Zungu na Najima Giga.
Katika hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais
Dkt. Magufuli, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Watanzania wote walimuombea alipokuwa kwenye matibabu nje ya nchi pamoja na
Madaktari waliomhudumia akiwa kwenye matibabu na kumshukuru Mungu kwa
kumwonesha upendo alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.
Katika mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14
ambayo yalielekezwa kwenye Wizara mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea
ufafanuzi masuala yanayotekelezwa kwa Serikali