SAKATA LA MBOWE WA CHADEMA KUDAIWA BILIONI 1.3,NHC YATOA UFAFANUZI,SOMA HAPO KUJUA
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua
ya kufungia Kampuni ya Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa
Chadema Taifa si ya kisiasa, anaandika Pendo Omary.
Leo NHC kupitia wakala wake
Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo
katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es
Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.
Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai
kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa
licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.
Ndani ya Hampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media
inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.
Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji
Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni
ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.
Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema
asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo
kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala
la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.
“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu.
Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda
mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.
Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya
Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba
hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka
hapo deni hilo litakapolipwa.
Post Comment