RAIS KIKWETE AWAKIMBIA WAANDISHI WA HABARI UGHAIBUNI,SOMA HAPO KUJUA
RAIS Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, amekataa
kuzungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani huku msaidizi wake
akiwapiga vikumbo waandishi hao ili wasimsumbue ‘bosi’ wake, baada ya kutoka
katika mkutano wa 71 wa Umoja wa Mataifa, anaandika Charles William.
Mkutano huo ulioanza jana mjini
New York, unajadili masuala mbalimbali ikiwemo vita dhidi ya ugaidi pamoja na
utolewaji wa misaada zaidi kwa wakimbizi.
Mkanda wa video uliopatikana leo, umemuonyesha
Dk. Kikwete akitoka katika eneo la mkutano huku wandishi wa habari
wakijaribu kumuhoji lakini akikataa na kuendelea kutembea, akiondoka katika
eneo hilo.
Baada ya Dk. Kikwete kukataa kuhojiwa alionekana
akiwatupia maneno waandishi hao. Hata hivyo maneno hayo hayakuweza kunaswa na
vinasa sauti vya wandishi hao huku msaidizi wake akiwazuia waandishi hao ili
wasiendelee kumsogelea.
Haikujulikana mara moja, kwanini Dk. Kikwete
alikataa kuzungumza na wandishi wa habari katika eneo la nje ya mkutano huo,
ikizingatiwa kwamba katika siku za nyuma amekuwa ‘rafiki’ kwa waandishi.
Dk. Kikwete amehudhuria mkutano huo akiwa ni Balozi
wa heshima wa chanjo duniani na Mwenyekiti mwenza wa jopo la watu mashuhuri duniani
lenye jukumu la kumshauri Katibu Mkuu wa UN juu ya uboreshaji wa malengo ya
maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals).
Si Dk. Kikwete pekee ‘aliyewachomolea’ waandishi wa
habari, isipokuwa hata Christine Lagarde, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
fedha ya kimataifa (IMF), naye hakuwa tayari kuzungumza na wanahabari baada ya
kutoka katika mkutano huo.
Mkutano huo wa 71 wa UN umeendelea tena leo ambapo
Rais Barrack Obama wa Marekani, amehutubia akizungumzia suala la kuongeza
misaada kwa wakimbizi ikiwemo utolewaji wa elimu kwa wakimbizi