MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YASHUKA KWA ASILIMIA 81,MARRY KINABO ASEMA CHANZO,SOMA HAPO KUJUA
Idadi ya mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeshuka kwa
asilimia 81 kutoka bilioni 9 na kufikia 1.7 bilioni katika kipindi cha wiki
iliyopita.
Hayo yamesemwa leo na Afisa
Masoko Mwandamizi wa DSE Marry Kinabo wakati akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam.
“Idadi ya mauzo imeshuka kwa
asilimia 81 kutoka bilioni 9 na kufikia 1.7 bilioni, pia idadi ya zilizouzwa na
kununuliwa zimeshuka kwa asilimia 68 kutoka milioni 1 hadi 340,000,” amesema.
Amesema pia ukubwa wa mtaji wa
soko umeshuka kwa asilimia 2.79 kutoka trilioni 21 na kufikia 20.7 trilioni.
Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kilekile cha Panda
8.2 trilioni.
Aidha, Kinabo ametaja kampuni
tatu zilizoongoza kwa idadi ya zilizouzwa na kununuliwa katika kipindi cha wiki
iliyopita kuwa ni CRDB kwa asilimia 53, TBL asilimia 35, na Swissport kwa
asilimia 3.
“sekta ya viwanda wiki
ilkyoisha imeshuka kwa alama 36.6 baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa
asilimia 1.08. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha imepanda kwa pointi 3.64
baada ya bei kpanda kwenye kaunta za DSE kwa asilimia 11.57,” amesema.
Pia amesema sekta ya huduma za
kibiashara kwa wiki iliyopita imeshuka kwa pointi 4.19 baada ya bei kupanda
kwenye kaunta za Swissport.