HABARI MUHIMU KUTOKA KWENYE MFUKO WA HUDUMA ZA KISHERIA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatilliaji wa Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Patience Ntwina akizungumza na watoa msaada wa kisheria leo jiji Dar es Salaam. |
Imeelezwa kuwa watoa msaada wa kisheria wanaumuhimu katika kuwasadia wananchi kupata haki pale wanapokuwa na tatizo la kiseheria.
Hayo ameyasema leo Mkurugenzi wa Katiba na Ufatilliaji wa Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria, Patience Ntwina,wakati wa utoaji wa mfano wa hundi kwa watoa msaada wa kisheria iliyotolewa na Mfuko Huduma za Kisheria (S.L.F)
Amesema kuwa wanaotoa msaada wa kisheria katika kufanya kazi kwa ufanisi.
Ntiwina amesema kuwa kwa mfuko huo kutoa bilioni 19 kwa watoa msaada wa kisheria katika kutimiza miaka mitano wamesaidia wananchi katika kuweza kupata kazi.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo na Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Joaquine De Mello amesema kuwa wakati wakifanya ziara magerezani wamekuta robo tatu ya walio magerezani ni watuhumiwa tu.
Amesema kuwa wanamuunga mkono , Mchungaji Kiongozi, Mama Getrude Lwakatare kwa kuwatolea dhamana watu hao na wengine wanatakiwa kwenda na kuanza kuuliza kwa katika vituo vya polisi .
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko huo, Scholastica Jullu amesema kuwa wanaotoa msaada wa kisheria wanaonekana watu wasio na thamani lakini ndio wamekuwa wakisaidia watu katika kupata haki.
Amesema kuwa kwa hali iliyofikia kunahitajika kuwepo kwa chombo cha serikali katika kuwaratibu wanaotoa msaada wa kisheria katika kufikia malengo ya ufanisi wa utoaji haki. Amesema wametoa billioni 20 kwa taasisi