BAADA YA SERIKALI KUANGUKIA PUA SAKATA LA ESCROW NA KUAMULIWA KULIPA MABILIONI TENA,ZITTO KABWE AMVAA RAIS MAGUFULI ASEMA AMEYATAKA,SOMA HAPO KUJUA
Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL?
Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki
ya Standard Chartered ilipwe Shilingi Bilioni 300 na riba. Kiwango Hicho Ni
zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda.
TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa
Fedha za TEGETA Escrow na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala
hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais Kwanini hashughulikii Ufisadi huu wa
IPTL/PAP? Nini Kinamzuia Rais Kuchukua Hatua dhidi ya Wizi huu wa Dhahiri Kwa
Taifa?
Tanzania Tunapata Hasara mno, Na Hizi zote Ni Fedha
za Wananchi zitakazopotea.
• Watanzania mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa
kwenye "TEGETA escrow account", Fedha ambazo ziligaiwa Kwa Viongozi
mbalimbali wakiwemo Mawaziri.
• Watanzania Mmewapa Mtambo wa kuzalisha umeme
matapeli hao na mnaendelea kuwalipa "capacity charges" mpaka sasa -
Kinyume Kabisa na Maazimio ya Bunge yanayotaka Mitambo Husika itaifishwe.
• Baada ya Hukumu hii Watanzania tutawalipa Standard
Chartered Fedha zao kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo (Kama
tungelazimika Kulipa) tungezitoa kwenye Akaunti ya Escrow - Lakini sasa
tutazitoa Hazina zikiwa ni Kodi za Watanzania.
Ushauri Wangu - Rais achukue Hatua Zifuatazo:
• Awafikishe Mahakamani watu wote waliohusika na
kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow.
• Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha
Kwa TANESCO (Kama ilivyoazimiwa Na Bunge).
• Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi
wake wote na kuwafikisha Mahakamani Kwa makosa ya Utapeli, Wizi, Uhujumu
Uchumi, Utakatishaji wa Fedha nk.
• Ahakikishe Taifa halilipi Fedha Hizi Kwa Standard
Chartered. Benki iliyotumika Kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo
deni tunalotakiwa kulipa.
MUHIMU: Rais AAMUE Kusimama na WATANZANIA au
kusimama na "Matapeli wa TEGETA escrow".
Zitto Kabwe Ruyagwa
Sept 19, 2016
Sept 19, 2016