KAMPUNI YA KUJENGA BARABARA YA DEL-MONTE YAENDELEA KUKATALIWA JIJINI DAR,NAIBU MEYA WA ILALA AUNGANA NA RC MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Ngumilamoto akifafanua jambo na waandishi wa habari(Picha na Maktaba) |
NAIBU meya wa Manispaa ya Ilala,Omary Ngumilamoto
amesema wataiondoa kwenye tenda Kampuni ya ujenzi wa Barabara Del-Monte
katika manispaa hiyo baada ya kujiridhisha kampuni hiyo inafanya kazi
chini ya kiwango ikiwemo kuchelewesha kumaliza kazi kwa wakati.Anaandika KAROLI
VINSENT endelea nayo,
Kauli ya Ngumilamoto inakuja ikiwa ni tayari mkuu wa
mkoa wa Dare s Salaam,Paul Makonda ambaye naye aliiagiza viongozi wote wa
manispaa ya mkoa huo kutoipa tenda kampuni ya Del-Monte kutokana na
kujenga barabara nyingi chini ya kiwango.
Ngumilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti
kupitia chama cha Wananchi (CUF) ameyasema hayo leo wakati alipokuwa anafanya
ziara na Kamati ya fedha ya Manispaa hiyo kwenye miradi mbali mbali iliyoanza
kutekelezwa ili kujilidhisha juu ya ufanisi wake.
Amesema Kampuni hiyo ilipewa tenda ya kujenga
barabara kutoka Mombasa hadi Mosha Baa kwa kiwango cha Lami ambayo inaurefu wa
kilomotea 1.65 ambayo itagarimu Bilioni Sh 2.4 ambapo kwa sasa kampuni
hiyo imepewa milioni 301,
“Hii Kampuni ya Del-monte tulishakamtaa kutokana na
miradi mingi tunayompa kushindwa kumaliza miradi kwa wakati licha ya
kupewa fedha lakini bado anatusumbua”amesema Ngumilamoto,
Ngumilamoto amesema Halmashauri hiyo ilishaingia
Mkataba na kampuni hiyo hivyo hawezi kumkatisha mkataba wake,ila amedai kuwa
Mkataba wake ukishamalizika hawataendelea nayo kampuni hiyo ikiwemo kuipa tenda tena katika Halmashauri hiyo.
Sanjari na hayo,pia Ngumilamoto amemtaka Kaimu
Mhandisi wa Manispaa hiyo,Nyamagulula Masatu kuhakikisha anasimamia miradi huo
uwe unakamilika kwa wakati na kuisimamia ipasavyo kutokana na kuwepo kwa miradi
mingi ya Barabara kuharibika hata mwaka mmoja haujamilizika.
Kwa Upande wake Mhandisi Masatu alimuhakikishia
Ngumilamoto kuwa ataisimamia mradi huo na kuhakikisha itaisha kwa
wakati.