FREEMAN MBOWE AANZA KUMUUMBUA MKURUGENZI NHC,MAHAKAMA YAZIDI MWEKA MSALABANI TARATIBU,SOMA HAPO KUJUA
Mahakama yatupilia mbali mapingamizi manne
yaliyowekwa na Mawakili wa shirika la nyumba la taifa(NHC) Katika kesi ya*
*MBOWE Hotels Ltd t/a BILLICANAS*
Mahakama kuu kitengo cha ardhi
imetupilia mbali mapingamizi manne ya kisheria yaliyowekwa na mawakili wa
Shirika la nyumba la Taifa (NHC) likiongozwa na wakili sekule.
Mahakama imeshawishika na hoja
zilizojibiwa na jopo la mawakili likiongozwa na *Peter Kibatala* Kuwa hoja hizo
hazina mashiko kisheria.
Judge wa Mahakama Kuu ameshawishika na
kesi mbalimbali ambazo zimetumiwa kushawishi mahakama isizitilie maanani
MAPINGAMIZI Hayo.
Imesema vifungu ni sahihi na njia
iliyotumiwa na mawakili wakiongozwa na *PETER KIBATALA* ni sahihi
Pia Kuhusu Mkataba imesema hilo suala linabishaniwa
na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi kulichukulia juu kama NHC
wanavyotaka
TENA Kuhusu madai ya NHC kuwa Mkataba wa umiliki wa
pamoja(JOINT VENTURE) wa Jengo kati yake na Mbowe kumalizika 2015; mahakama
imesema hilo suala linabishaniwa na linahitaji ushahidi na Mahakama haiwezi
kulichukulia juu kama NHC wanavyotaka
Judge amesema ameshindwa kushawishika na hoja na
hata sheria ambazo mawakili wa shirika la nyumba wamezitumia.
Kesi hiyo itaendele tarehe 27/9/2016 katika mahakama
hiyo kwa kusikiliza maombi ambayo Mawakili wanomuwakilisha Mbowe Hotels
Ltd
Ambayo mojawapo ni kurudisha vitu ambavyo NHC na
Dalali wamevitoa sehemu yenye mgogoro kama ambavyo vilikutwa!.