Moja
ya Ahadi za Rais Magufuli alipokuwa kwenye majukwaa mbalimbali ya
kampeni ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya, na jambo
hilo limekuwa likifanywa na watendaji mbalimbali alio wateua kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Ambapo
siku ya leo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amekabidhi daipa elfu
85,000 kutoka Taasisi ya GSM Foundation katika Hospitali ya Amana Jijini
Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa Daipa hizo zitagawiwa katika vituo
vya afya 26 vya wilaya yake ambapo wazazi wenye watoto wanaohudhuria
kliniki na wale watakaojifungua hivi karibuni watakabidhiwa.
Aidha
Mkuu wa wilaya huyo ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha Huduma
za Afya, na kupongeza jitihada zinazofanywa na GSM Foundation huku
akiwataka wadau wengine waige mfano huo, na kuwaomba GSM Foundation
waendelee kuwasaidia kwani yapo masuala mbalimbali ya kiafya
yanayohitaji msaada wao.
2 Attachment
DC MJEMA AKABIDHI DAIPA 85,000 ZA GSM FOUNDATION, ZAIDI YA VITUO 26 KATIKA WILAYA YA ILALA KUNUFAIKA NAZO
Reviewed by Full habari Digital
on
19:48:00
Rating: 5