CHUO KIKUU CHA MLIMANI NA BILIONEA MO WAANZA MPANGO WA KUFADHILI WANAFUNZI,SOMA HAPO KUJUA
Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam – UDSM Imezindua rasmi mpango wa ufadhili kwa wanafunzi 10 wa elimu ya
juu waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2016 (MO Scholar Program) kwa chuo
kikuu cha Dar es salaam leo Jumatano Septemba, 7 2016.
Mpango huu wa ufadhili kwa wanafunzi umelenga kuwawezesha
wanafunzi wenye sifa tatu, wasio na uwezo wa kujilipia ada ya chuo, wanafunzi
ambao wameshiriki vyema katika michezo na uongozi wakiwa shuleni na wanafunzi ambao
wamefaulu kwa kiwango cha alama 1 na 2 (division 1 & 2)
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez amesema kuwa
wameanzisha mpango huo kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa
kutoa msaada wao wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi waliomaliza kidato
cha sita.
Mkuu
wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez akielezea jinsi wanafunzi
hao 10 watakavyoweza kufaidika na udhamini wa Mo Dewji Foundation.
“Mpango
wetu kwa muda wa miaka mitatu hadi minne ni kusaidia zaidi Tanzania
lakini hapo baadae kama tukifanikisha malengo yetu Tanzania tutakwenda
mbali zaidi,” ameongeza Barbara.
Aidha
Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Profesa Allen Mushi ameelezea kuwa chuo kikuu cha Dar es salaam
kimelenga kusaidia wanafunzi wote wa kitanzania ambao wanasifa za
uhitaji wa ufadhili na ameomba vyombo vya habari visaidie kusambaza
ujumbe kwa watanzania ili wanafunzi wafaidike na mpango huo.
Mkurugenzi
wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Profesa Allen Mushi akizungumzia mchakato wa kupata wanafunzi 10 ambao
watapata udhamini wa Mo Dewji Foundation.
“Tumeanza
na chuo Kikuu cha Dar es salaam, tutaangalia namna ambavyo mpango na
tutaenda na hapo baadae tutatanua mikono yetu kwenda vyuo mbalimbali,”
amesema Barbara.
Mkurugenzi
wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Profesa Allen Mushi na Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez
wakipongezana mara baada ya kufanya uzinduzi.
Na
kwa mtahiniwa ambaye anakuwa anahitaji kutuma maombi kwa ajili ya kupata
ufadhili wa Mo Dewji Foundation kwa ajili masomo ya chuo kikuu anaweza
kuingia tovuti ya modewjifoundation.org
Baadhi
ya watumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na waandishi wa habari
waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa UDSM.