CHADEMA YAFUKUZA DIWANI WAKE KWA UFISADI,SOMA HAPO KUJUA
September
19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke
kimemfukuza uanachama Diwani na Mwenyekiti wake kutoka kata ya Kurasini,
Matiti Claudian Togocho kutokana na kashfa ya ufisadi wa zaidi ya
shilingi milioni 400 alizozipata kwa njia ya udanganyifu.
Taarifa
iliyotolewa na Benard Mwakyembe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya
ya Temeke imeeleza kuwa mnamo November 23 2015, Diwani huyo akiwa na
wenzake wanadaiwa walitengeneza hati feki ya nyumba tano za James
Makundi aliyekuwa mpangaji kwenye nyumba zake kisha kufanya hujuma ya
kuvunja nyumba hizo kwa amri ya uongo ilitolewa na wakili kishoka wa
Samora Avenue badala ya amri ya mahakama ikiwa ni kwa lengo la kujipatia
pesa kutoka kwa mwekezaji ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.
Diwani
huyu pia anahusishwa na matukio mengine mawili ya udhulumaji wa zaidi
ya shilingi milioni 140 za mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni
wakati kesi ikiwa mahakamani pamoja na fedha za fidia za Paulina Shaban
na wajukuu zake ambao Diwani huyo alisimamia nyumba zao kubomolewa.
"Kutokana
na maamuzi ya chama baada ya kujiridhisha na makosa yake na kwa mujibu
wa katiba ya chama chetu, mamlaka za mwisho zimefikia maamuzi ya kumvua
uanachama wake hivyo atakuwa amepoteza sifa za kuwa Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa wa Mivinjeni pamoja na nafasi yake ya Udiwani kata ya
Kurasini." Alisema Benard Mwakyembe