Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla afungua mkutano wa wadau dhidi ya Mapambano ya Sumukuvu,soma hapo kujua
Serikali imesambaza chakula salama na kutoa tiba bure kwa
waathirika wa ugonjwa wa mlipuko wa sumukuvu katika mikoa ya Dodoma na Manyara
uliotokea hivi karibuni.
Hayo yamesemwa mapema leo
Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Hamisi Kigangwalla wakati wa uzinduzi wa mkutano wa
watafiti wa chakula uliojadili madhara na athari za sumukuvu.
Dkt. Kigwangalla alisema
Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapelekea vyakula salama waathirika wa ugonjwa
huo na kuteketeza vyakula vyenye sumukuvu.
“Tumepanga utaratibu wa
kupeleka vyakula salama kwa waathirika wa ugonjwa a sumukuvu katika mikoa
husika bila malipo ili kusaidia kuondoa ugonjwa huo na kuteketeza mabaki ya
vyakula vyenye vizaria vya sumukuvu” alisema Dkt. Kigangwalla.
Aidha Dkt. Kigwangalla alisema
kuwa Serikali ipo bega kwa bega na waathirika wa sumukuvu ili kuhakikisha
wanaondoa ugonjwa huo kwani tayari umethibitishwa na wataalamu na unapatikana
kwenye mazao ya vyakula kama vile mahindi, uwele, mtama na karanga.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigangwala
alisema katika kukabiliana na ugonjwa huo Serikali imeamua kushirikiana na
wataalamu wa kimataifa ili kuweza kuondoa ugonjwa huo kwenye vyakula
vinavyolimwa nchini ili kuyawezesha mazao mazao hayo kuuzwa kwa urahisi hapa
nchini.
Dkt Kigwangalla aliwashukuru
watafiti hao kwa kugundua chanzo cha ugonjwa huo ambao unasababishwa na Jamii
ya fangasi wanaoitwa Aspergillus wanaojikita zaidi kwenye vyakula na kuwataka
wapate matokeo chanya ya kutokomeza sumukuvu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Silo alisema katika mkutano huo watafiti
hao wanatarajia kujadili na kupata ufumbuzi wa tafiti za vyakula mbalimbali ili
visiendele.