Agosti
15 Mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alionyesha
dhamira yake ya kutaka kujenga Ofisi za Makao Makuu ya Baraza la Kuu la
Waislamu Nchini (BAKWATA), baada ya kukabidhi ramani ya jengo la ofisi
hizo kwa Muft Mkuu wa Tanzania Abubakari Zuberi na kuhaidi kukamilika
kwa jengo hilo ndani ya miezi 14, ambapo zilizuka hoja kuwa hatoweza
kutekeleza kwa kuwa amahaidi mengi na hajayatekeleza kikamilifu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam zilizopo ofisi hizo za BAKWATA Makonda ameeleza
kuwa wanaopinga jitihada zake wanawivu usiokuwa na tija kwani yeye ni
kiongozi wa watu wote wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kujali dini, rangi,
jinsia, kabila na itikadi za kisiasa, hivyo atahakikisha wote wanapata
haki sawa lakini ameamua kuanza na viongozi wa dini kwa kuwa wanastahili
kuenziwa, kuheshimiwa kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya kulinda,
kuombea amani na kuwa amrisha mema waumini wao.
Huku
akieleza kuwa katika jitihada hizo za ujenzi wa ofisi za BAKWATA,
amepata ufadhili kutoka Taasisi ya GSM Foundation ambao watalijenga
jengo hilo la ghorofa tatu litakalo gharimu Shilingi Bilioni 5 na
milioni 200, kwa muda wa miezi 14 kama alivyo agiza Mkuu wa Mkoa Makonda
wakija na ramani tofauti na jengo lililokusudiwa awali, huku likiwa na
nguzo tano kama ilivyo Dini hiyo ya Kiislamu, Ukumbi wa Mikutano,
Maktaba, Kompyuta,lifti, ofisi za kisasa za Mufti zikiwa nne katika
ghorofa ya tatu na ofisi nyingine ya Sheikh Mkuu wa Mkoa, Katibu Mkuu wa
BAKWATA,Kadhi, Baraza la Maulamaa, kumbi za wanawake.
RC MAKONDA ATEKELEZA AHADI YAKE KWA WAISLAM,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:44:00
Rating: 5