RC MAKONDA AAGIZA POLISI KUPIGA WAHALIFU,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wahalifu wowote wakiwamo
majambazi pindi wanapowakamata.
Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari watatu
kati ya wanne wa Jeshi la Polisi waliouawa wiki hii katika tawi la benki ya
CRDB lililopo Mbande wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda alisema
jambazi atakapokutwa popote iwe msituni iwe wapi agongwe na apigwe.
Alisema alipopata taarifa ya vifo vya askari hao
wanne alifungua pazia za madirisha nyumbani kwake na kuwaangalia askari
wanaolinda na kulia kwa uchungu na kwamba usiendelezwe ukichaa wa haki za
binadamu kwani ni uendawazimu ambao hauwezi kuvumilika.
“Kamanda Sirro (Simon) mimi ndiyo mkuu
wako wa mkoa nasema ukikamata hao watu popote gonga, piga na watu wa haki za
binadamu wakija waambie waje kwangu, hatuwezi kukaa kwenye mkoa ambao haupo
salama,” alisema Makonda aliyedai hana maneno
mazuri ya kusema kwa sababu hakuumbwa kumfurahisha mtu, bali anafanya kazi ya
Mungu na wakati wake ukiisha ataondoka.
“Kama kuna haki za binadamu nataka
haki za askari wangu kwanza. Kama hao watu wa haki za binadamu wapo nataka
kuona wakiandamana kukilaani kitendo hiki, ”alisema
Makonda.