FREEMAN MBOWE AMEJAA BUSARA,HATUA YA KUSITISHA UKUTA,WANANCHI WAMFAGILIA KILA KONA NA WAMUONYA JPM,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa chama
cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni
UKUTA yaliyokuwa yamepangwa
kufanyika kesho nchi nzima.
Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha maandamano mchana huu wakati akiongea na vyombo mbalimbali vya habari.
Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara zaviongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu
Mbowe amesema maandamano hayo yameahirishwa hadi Oktoba Mosi ili suluhu ipatikane kwa viongozi wa dini watakapokwenda kukutana na Rais John Magufuli

WANANCHI WAMPONGEZA MBOWE.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wananchi mbali mbali wampongeza Mwenyekiti huyo ambaye ni mbunge
wa Jimbo la Hai wamesema hatua ya kuzuia maandamano ni jambo jema huku
wakisema mwenyekiti huyo ni mtu makini
na ni mlezi wa amani ya Tanzania.
Ally Salum Ally mkazi
wa Magomeni amesema licha ya viongozi wa serikali ya awamu ya tano kusinya
katiba ya Jamhuri wa Muungano lakini bado vyama vya siasa kikiwemo chadema
kuonyesha utulivu wa kisiasa.
Amefafanua kuwa hatua
ya serikali kuminya katiba jambo hilo lingetokea katika nchi zengine basi amani
ya Tanzania ingekuwa rehani.
Hata hivyo Ally
amemuomba Rais John Magufuli kuwasilikiza kwa makini viongozi wa dini pindi
wakimtembelea na akubali kutafuta suluhu la vyama vya siasa kwani bila siasa
makini basi serikali ya viwanda anayoitaka, ataishia kuiimba jukwaani.
"Huyu mbowe ni mtu makini sana na amewasilikiza viongozi wa dini,kwani mtu mwenye maono uwasikiliza viongozi wa kiroho,na mbowe ameonyesha umakini wake,hata sisi tunamuomba Mungu ampe nguvu mbowe aendelea kuwa na uvumilivu kama huu.na tunamuomba Rais Magufuli naye aige mfano wa Mbowe"amesema Joseph Kesi mkazi wa Morogoro