DK MAHANGA AMLIPUA JAMES LIMBELI,NI KWA HATUA YAKE YA KUJIKOMBA KWA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
James Lembeli (katikati) akifurahia jambo na Rais John Magufuli walipokutana Kahama |
JAMES Lembeli amesikitisha wengi. Kauli yake ya
kumshabikia Rais John Magufuli imeibua mjadala kwamba, ni mpinzani ama
mamluki?, anaandika Charles William.
Kwa muda wa miezi kadhaa
Lembeli alikuwa kimya, lakini ghafla aliibuka katika mkutano wa Rais John
Magufuli na wananchi wa Kahama mkoani Shinyanga na kuanza ‘kujikomba.’
“Nipo
hapa kwasababu kazi unayoifanya sasa hivi mheshimiwa rais, ndiyo kazi ambayo
kwa miaka 10 nikiwa mbunge niliipigania, lakini siwezi kurudi kundini mpaka
umesafisha chama kile.”
Hiyo
ni kauli ya Lembeli mbele ya Rais Magufuli pia Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM)-Taifa ambaye alimpa Lembeli nafasi ya kusema jambo kwenye
mkutano huo.
Ikiwa
ni siku moja tangu Lembeli ambaye alikuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Kahama, Shinyanga kumshabikia Rais
Magufuli, Dk. Makongoro Mahanga amesema, ni upuuzi mtupu.
Dk.
Mahanga, aliyekuwa Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na baadaye
kujiunga na Chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana amesema, hakutarajia
Lembeli kutoa kauli tata ya kumshabikia Rais Magufuli.
Kauli
hiyo imeonekana kuchefua wengi miongni mwao akiwa Dk. Mahanga ambaye amesema,
“rafiki yangu wa siku nyingi Lembeli, kaninyong’onyesha sana, hivi hajui kuwa
mazuri yoyote ambayo Magufuli anayafanya, yanafutwa kabisa na utawala wa
kidikteta pamoja na uminyaji wa demokrasia?”
Dk.
Mahanga amesema, inasikitisha kuona Lembeli akisifia kazi za Rais Magufuli
wakati anajua wazi kuwa, miongoni mwa kazi hizo kwa sasa ni pamoja na uminyaji
wa demokrasia na vitendo vya kidikteta.
“Lembeli
anaposifu kuwa, yanayofanywa na Rais Magufuli hata yeye alikuwa anayapigania
miaka 10 iliyopita, ina maana Lembeli alikuwa anapigania nchi hii iendeshwe
kibabe, kidikteta na kwa kufinyanga demokrasia?,” amehoji Dk. Mahanga kupitia
ukuraa wake wa facebook.