CHADEMA YAAENDELEA KUTESEKA,MADIWANI WAKE WAENDELEA KUKAMWATWA,SOMA HAPO KUJUA

Madiwani watatu wa Chadema na mfuasi mmoja wa chama
hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rombo kwa makosa ya kufanya
uchochezi.
Madiwani hao, Nicolaus Kimario (Kirio), Anasia
Kimario (Viti Maalumu), Daud Tarimo (Leto ) na mfuasi wa Chadema, Rogath Kanje
walikana mashtaka hayo.
Mwendesha mashtaka, Bernard Machivya alieleza
mahakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 25, wakiwa nyumbani kwa
mmoja wa washtakiwa Nicolaus Kimario.
Aliieleza Mahakama kuwa washtakiwa wote wanne
walitenda kosa hilo kwa pamoja wakifanya vikao vya kuhamasisha wananchi
wajitokeze kwenye maandamano ya Ukuta Septemba Mosi.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Rombo,
Naomi Mwerinde aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 5 na watuhumiwa wote
wataendelea kukaa rumande.