BREAKING NEWS,WAZIRI NAPE AIFUNGIA REDIO YA LOWASSA,PIA AMEIFUNGIA MAGIC FM,KISA HICHI HAPA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI wa Habari,utamaduni ,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye amevifungia kwa mda kwaanzia leo, kituo cha redio Five cha Arusha ambayo ni mali inayomilikiwa na Waziri mkuu wa
Zamani Edward Lowassa pamoja na kituo cha Redio cha Magic Fm kwa kile
kinachodaiwa vituo hivyo kurusha vipindi vyenye uchochezi.
Kufungiwa vituo hivyo inakuwa ni mwendelezo wa
Waziri huyo kuvifungia vyombo vya habari nchini,ambapo
kwa kipindi cha miezi nane cha Nape awe waziri katika wizara baada ya kuanza kuyafungia magazeti ya Mawio,Mseto yote yanayomiliwa na Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea
kwa hoja kuwa yanaaandika habari za Uchochezi.
Waziri Nape ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari ametangaza
kuvifungia vituo hivyo vya redio leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na
waandishi wa habari amesema kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 28(1)
cha sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya mwaka 2003 imempa
mamlaka ya kuvifungia vituo hivyo,
Amesema Uamunuzi wa kuvifungia vituo amefikia baada
kujiridhisha kuwa Redio five katika kipindi cha matukio kilichorushwa tarehe 25 Agosti,2016 muda wa saa 2;00 usiku
hadi saa 3;00 usiku ambapo katika
kipindi hicho alimuhojiwa Mbunge wa Arusha Majini,Godbless Lema ambapo alikuwa
anatoa maneno anayosema ni uchochezi.
Amesema licha ya Mbunge huyo kutoa lugha hizo,lakini
watangazaji wa kipindi hicho walishindwa kumsahihisha jambo analodai linakwenda
kinyume na sheria ya utangazaji.
Mbali na Redio hiyo inayomilikiwa na Lowassa ambaye
ni Alikuwa ni mgombea wa Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema kwenye uchaguzi uliopita pia ametaja kosa lilipelekea kukifungia kituo
cha Magic Fm cha Dar es Salaam.
Amedai mnamo tarehe 17,Agosti 2016 katika kipindi cha
Morning Magic kipindi hicho kilichoruka
mda saa 1.00 asubuhi na saa 2.30 katika kipengele cha Kupanga
Rangi watangazaji wa kipindi hicho walisikiaka wakitoa maneno anayoeleza kuwa
ni ya uchochezi.
“Watangazaji hawa Magic walisema kama Rais anavunja
Katiba sasa wananchi wa chini wafanyaje,nao lazima watafanya hivyo,”Amesema
Nape.
Amesema baada ya kuvifungia vituo hivyo kwa mda
ambayo hajautaja ni lini,ameitaka kamati ya Maudhui ya (TCRA) kukutana ili waziite
pande zote mbili za redio hizo ili waweze kujitetea.
Amesema kamati hiyo ikishakutana na kusikiliza
utetezi wa redio hizo, basi yeye atachukua hatua ya kuvifungulia au kuendelea
kuvifungia.