TRA YAZISHUKIA BENKI NCHINI,NI ZILE ZILIZOANZA KUWAKATA WATEJA WAKE KODI MPYA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),Alpayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari |
NA KAROLI VINSENT
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imezitaka baadhi ya
Benki nchini ambazo zimeanza kuwakata kodi ya asilimia 18 wateja wao kuacha
mara moja.
Huku Mamlaka hiyo ikitishia kuwasiliana na Benki kuu
nchini (B.O.T) ili iweze kuzichukulia hatua kali benki hizo kwa kile wanachokiita benki zinafanya utapeli kwa wateja wake.
Hayo yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna
mkuu wa (TRA),Alpayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari ili
kutolea ufafanuzi hatua ya benki hizo kuanza makato hayo kwa wateja wake,
Ambapo amesema amesikitishwa na hatua ya benki hizo
kupokea vibaya marekebisho ya sheria ya
kodi ya ongezeko la thamani ya (VAT) ya mwaka 2014 ambayo imepitishwa na Bunge hivi karibuni, kwa hatua ya kuwapelekea mzigo wateja
wao wakati ni kinyume na sheria inavyotaka.
Kidata amefafanua kuwa sheria hiyo inalenga kutoza
kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia 18 ya kwenye ada (fees) ambazo benki
hizo inatoza wateja wake kwenye huduma mbali mbali za kibenki.
“Mfano ada (fees) ya huduma ya kibenki ambayo mteja
ametozwa ni shilingi 1000/- kodi ya ongezeko la thamani itakayotozwa kwenye
kiasi hiki ni shilingi 152.50 tu na benki kubaki nashilingi 847.50,huku kiwango
cha 152.50 kinalejeshwa serikalini,sasa tunashangaa leo hizi benki zinaanza
kumtoza mteja wakati sio kweli”ametolea mfano Kidata.
Kitada ,amesema hata maelekezo yaliyotolewa na benki
moja hapa nchini kuwa mtumiaji wa huduma za kifedha atatakiwa kulipia kwa fedha
taslimu kama muamala husika kupitia kwenye akaunti, amedai taarifa hiyo si sahihi
kwa kuwa ukusanyaji wa VAT husika utafanywa kwa njia ya ile ile ambayo gharama
za huduma za kifedha zinakusanywa sasa.
Hata hivyo,Kidata amesema endapo Benki hizo zikizidi
kuendelea kufanya upotoshaji kwa kuendelea kuwakata wananchi fedha basi mamlaka
hiyo itawasiliana na Benki kuu ambao kimamlaka ndio wanajukumu la kusimamia
benki nchi ili hatua kali zichukuliwe.
“Harafu toka lini benki hizi zikaanza kutangaza
hadharani kuwa zinaanza kukata kodi kwa wateja wake,wakati kihistoria hazijawai
kufanya kitu kama wanachokifanya sahivi,na ukiona wanafanya hivyo sasa mfahamu
kuwa hapa wanajua wanafanya upotoshaji na sisi tutawasilina na benki kuu ili
wazichukulie hatua.”amesema Kidata.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni