MAELFU WAJITOKEZA DAR KUWALILIA WAPALESTINA…SHEIKH JALALA AONGOZA MATEMBEZI
Ikiwa
ni siku mbili tokea Kiongozi mkuu wa Dhehebu la shia Ithnasheriya kuwatangazia
umma wa watanzania wanaopenda Amani kujitokeza
kwa wingi kushiriki matembezi ya Amani, Maelfu wameitikia wito huo na
kujitokeza kushiriki matembezi hayo.
Fullhabari.com
imeshuhudia wakazi wa Jiji la Daresalaam wakiacha shughuli zao na kushiriki
maandamano hayo yaliyoanzia Ilala boma na kuishia katika msikiti wa Al Qadir
Kigogo Jijini Daresalaam.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa nyakati tofauti, mmoja wa wananchi walioshiriki matembezi
hayo, Bw. Yasini Kasim amesema awali ilikuwa ni vigumu kuelewa uzito wa
matatizo wanayofanyiwa Waislamu wenzao wa Palestina lakini kutokana na taarifa
ambazo wanazipata kila leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari amejikuta
amevutiwa na kuona umuhimu wa kupinga dhulma inayofanywa huko Palestina.
Kasimu
alisema anawashukuru uongozi wa msikiti wa Al Qadir Kigogo kwa jitihada
wanazozifanya za kutoa elimu kwa umma kuhusu suala la Palestina, kwani taratibu
suala hilo limeanza kueleweka katika jamii ya watanzania.
“Wakati
nipo katika gari nilisikia watu wakisema hivi hawa watu kimewakuta nini, suala
la Palestina wao linawahusu nini, hawa huenda wanauhusiano na makundi ya
Alshabab hivyo wanaweza kuleta vurugu na kupoteza Amani iliyopo Tanzania, hapo
niliona kuwa licha ya elimu kuanza kuonekana kuenea lakini viongozi hawapaswi
kubweteka kwani bado kuna kundi kubwa linalohitaji elimu”Alisema Kasim.
Naye
Salim Abdallah Mkazi wa Luhanga jijini
Daresalaam amesema vitendo wanavyofanyiwa Waislamu wa Palestina ni vya
kizalilishaji na uonevu wa hali ya juu hivyo ni vyema wale wanaopenda Amani duniani
wachukue hatua mapema kumaliza shida iliyoko Palestina.
SHEIKH
JALALA AZUNGUMZA
Kwa
upande wake kiongozi mkuu wa dhehebu la
shia Ithnasheriya, Sheikh Hemed Jalala amesema wamefarijika kuona kuna watu
wamewaunga mkono katika matembezi hayo na kwamba hiyo ni sihara kuwa watanzania
wanapinga vitendo vya dhulma vinavyofanyika na wazayuni huko Palestina.
Amesema
watanzania wanapaswa wafahamu kuwa suala la Palestina linashabihana kwa karibu
na kulinda Amani Duniani, kwa hiyo kupinga dhulma dhidi ya Wapalestina ni
sawasawa na kupigigania Amani Dunia.
Amesema
athari ambazo zinajitokeza Palestina zinatisha, sasa Wapalestina wamekuwa kama
wakimbizi katika Taifa lao, jambo ambalo si haki kwani wanastahili kuachiwa
maeneoa yao ili waweze kuishi kwa Amani kama Tanzania nan chi zingine Duniani
zinavyofanya.
Matembezi
ya Amani ya Quds yanafanyika kila Ijumaa ya wiki ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa
Ramadhani, lengo likiwa ni kuwaunga mkono Waarabu wa Palestina wanaodhulmiwa
mali zao, ardhi yao na kubomolewa makazi yao. Mpaka sasa tayari jumba Zaidi ya
Elfu 45 zimeshabomolewa toka mwaka 1967.
SHEIKH HEMED Jalala akiongoza matembezi ya amani. |
MATEMBEZI YA QUDS MAPEMA HII LEO. |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni