AMANA BENKI WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA
Mkuu wa biashara wa AMANA BENKI Bw. Munir Rajab akifafanua jambo kuhusu kituo hicho. |
NA SELEMANI MAGALI- DARESLAAM
BENKI ya Kiislamu ya
Amana imezindua kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa
kuboresha huduma kupitia teknolojia ya mawasiliano
Akizungumza na waandishi
wa habari Jijini Dar es Salaam,Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa
Benki hiyo Bw. Juma Msabaha alisema uzinduzi wa kituo hicho umelenga kuboresha
mahusiano ya wateja pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.
Akifafanua kuhusu kituo
hicho, Bw. Msabaha alisema kituo hicho kitafanya kazi kwa masaa 15 kuanzia saa
mbili asubuhi hadi saa nne usiku ambapo wateja wa Amana na ambao bado
hajabahatika kutumia huduma za benki hiyo watapata fursa ya kuuliza masuala
mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Benki.
“Tumejipanga vizuri,
tunayo timu nzuri yenye uzoefu na masuala ya Kibenki ,watafafanua mambo
mbalimbali kuhusu huduma za Amana benki kuanzia masuala ya akaunti,miamala ya
kimtandao na huduma zinazotolewa na mawakala wetu kote nchini.Alisema Msabaha.
Ameongeza kusema Kituo hicho
kitafanya kazi siku saba katika wiki,pamoja
na siku za siku kuu jambo ambalo wanaamini litasaidia kufafanua mambo
mbalimbali yanayowahusu wateja.
“Namba yetu ya huduma kwa
mteja ni 0657 980 000, kupitia namba hiyo ni matarajio yetu kuwa wateja
watafurahia zaidi huduma tuliyoizindua kwani ni rafiki kwa kila mmoja,
imeandaliwa mahususi kabisa kuwapa uwezo wananchi kupiga simu,kutuma ujumbe
mfupi pamoja na njia zingine za mitandao ya kijamii”.Alisema Msabaha
Kwa mujibu wa Bw Msabaha kituo
hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara
kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri
kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri
Alibainisha kuwa huduma
hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa
inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi yao hatua
aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja wake
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Biashara ya Amana
Benki Bw. Rajab Munir amesema wateja wa Amana watapata fursa ya kuijua benki
yao kwa undani kwani sasa wanaweza kuulizwa maswali yao na kujibiwa kwa wakati
ndani ya masaa 15 katika wiki ikiwamo siku za siku kuu.
Alisema hiyo ilikuwa dhamira yao ya muda mrefu na
kuzinduliwa kwake imekuwa ni faraja kwa wateja ambao sasa watafaidika nayo.kwa
kupata majibu ya papo kwa hapo kuhusiana na akaunti zao, miamala yao na misaada
kuhusu kutumia huduma za kimtandao.
katika kipindi kisichopungua miaka mitano Tayari Benki ya Amana kwa imefanikiwa kuwa na matawi saba matano yakiwa katika Jiji la Daresalaam na mengine mawili yakiwa katika Jiji la Mwanza na Arusha.
Mipango ya Baadae ni kwamba Amana benki inatarajia
kufungua matawi mengine si chini ya matatu
kati ya Mkoa wa Tanga au Zanzibara kulingana na upembuzi yakinifu
utakaofanywa na benki hiyo.