ZITTO KABWE HANA MCHEZO,AMPOPOA TENA RAIS MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
ZITTO Kabwe, kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
ametoa tamko lake juu ya kauli ya Rais John Magufuli ya kupiga marufuku vyama
vya siasa kufanya shughuli za kisiasa zaidi ya bungeni na kwenye kampeni za
mwaka 2020 ni sawa na kuua demokrasia.
Kwa habari zaidi soma tamko la
Zitto Kabwe juu ya kauli hiyo hapa chini.
Kauli ya Rais John Magufuli kuzuia yyama
kufanya Siasa mpaka mwaka 2020.
Tumepokea
kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa
havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa kampeni na kupitia bungeni.
Tunaichukulia
kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi
nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya nchi na namna
ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu.
Tunatoa
wito kwa vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha
tunapigana vita hii pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa
kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote
kwa mujibu wa Sheria.
Tunatoa
wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara katika kulinda
demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa huwezi kuua
demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka
kuua demokrasia nchini mwetu.
Hatua
zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na mshikamano wa wananchi na
Taifa, ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yetu kijamii, kisiasa na
kiuchumi. Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika
kulinda demokrasia.
Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni