ZITTO KABWE AJILIPUA TENA BUNGENI,AWALIZA WABUNGE,SOMA HAPO KUJUA
ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo
amekoleza moto wa wabunge kukatwa kodi katika fedha za kiinua mgogo, anaandika Dany Tibason.
Wakati hayo yakifanyika,
Serikali ya Rais John Magufuli imewang’oa wabunge wa viti maalumu kushiriki
kwenye Kamati za Fedha na Mipango za Halmashauri.
Jumatano
wiki hii serikali ilisoma bajeti yake ya Sh. 29. 52 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17,
sehemu ya bajeti hiyo ilionekana kukera wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Mheshimiwa
spika, natangaza kufuta msamaha wa kodi ya mapato kwenye malipo ya kiinua
mgongo kinacholipwa kwa wabunge kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili
kujenga misingi ya usawa na haki katika utoaji wa kodi kwa kila mtu
anayestahili kulipa kodi,” alisema Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na
Mipango.
Kutokana
na mpango huo wa serikali kutoza kodi katika kiinua mgongo cha wabunge na kuzua
zogo kwa wabunge wa CCM, Zitto amesema, ni vema serikali ikafanya hivyo ili
kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi kwa ajili ya kuendesha nchi.
Zitto
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini amekwenda mbali zaidi na kusema
kwamba, Bunge halipaswi kuishia kwenye kodi hiyo pekee kwa kuwa, kuna kodi
nyingi za wabunge ambazo hazijaguswa.
Kauli
hio ni mwendelezo wa msimamo wake wa kupinga wabunge kulipwa posho za vikao vya
bunge. Katika kampeni yake kwenye Bunge la 10, Zitto hakufanikiwa kuondoa posho
hiyo.
Zitto
ametoa msimamo wake kuhusu kukata kodi wabunge wakati akitoa maoni yake kwenye
uchambuzi wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 ulioandaliwa na Kampuni ya
Ukaguzi wa Hesabu za KPMG juzi.
Hata
hivyo Zitto amesema kwamba, pamoja na serikali kuanzisha kiinua mgongo hicho
lakini hakuna sheria yoyote inayoruhusu kitu hicho kufanyika na hivyo kuonesha
kushangazwa na hatua hiyo.
Hatua
ya Zitto bila shaka itakoleza mjadala wa posho ambao tayari CCM wameonesha
kukerwa na hatua ya serikali kuanza kutoza kodi hiyo.
Wakati
Waziri Mpango akiwasilisha bajeti hiyo na kufikia kipengele kinachoelekeza
kuwa, kodi hiyo itaanza kukatwa, wabunge wa CCM ambao ndio pekee waliokuwa
bungeni, walianza kuguna hatua mbayo ilimlazimu Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika
wa Bunge kuingilia kati na kutuwatuliza.
Wakati
hayo yakiendelea, serikali imeendelea kuwakomba posho wabunge baada ya Seleman
Jafo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) kueleza kuwa, wabunge wa viti maalum ni marufuku kushiriki kwenye
Kamati za Fedha na Mipango za Halmashauri.
Jafo
amesema, kwa mujibu wa sheria za Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, wabunge
hao hawaruhusu kushiriki kwenye kamati hizo.
Na
kwamba, ili wabunge hao waweze kushiriki kwenye kamati hizo, inahitajika
kubadili sheria kwanza ili pendekezo hilo liweze kutekelezeka.
Jafo
ametoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la Martha Umbula, Mbunge wa Viti
Maalum (CCM) na kwamba, Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Halmashauri wametajwa
katika kifungu cha 75(6) cha sheria sura 287 Mamlaka za Wilaya na
kifungu
cha 47(4) cha Sheria Sura 288 Mamlaka za Miji.
“Kwa
mujibu wa sheria hizo mbili wajumbe wa Kamati hawatazidi theluthi ya Madiwani
wote isipokuwa Kamati ya Fedha na Mipango ambayo wajumbe wake ni wale
wanaoingia kwa nyadhifa zao,” amesema Jafo.
Amesema,
upatikanaji wa wajumbe wa kamati hiyo umefafanuliwa katika Kanuni za Kudumu za
Uendeshaji wa kila Halmashauri.
Ameaja
wajumbe wake kuwa ni Mwenyekiti au Meya wa Halmashauri, Makamu au Naibu Meya,
Mbunge au wabunge wa majimbo, wenyeviti wa kamati za kudumu na wajumbe wasiozidi
wawili.
Amesema,
wajumbe wa Kamati ya Fedha wataendelea kuwa hao waliotajwa katika Sheria na
Kanuni za Mamlaka za Serikali za Mitaa hadi hapo
sheria
itakapofanyiwa marekebisho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
Hakuna maoni
Chapisha Maoni