Zinazobamba

UONGOZI WA TRL WAJIVUNIA MAFAKIO KWA KIPINDI KIFUPI TANGU UINGIE MADARAKANI,SOMA HAPO KUJUA




UONGOZI  wa shirika la Reli ya kati nchini (TRL) umesema katika kipindi kifupi wameweza kuliweka shirika mahala pazuri.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Kaimu mkurugenzi wa (TRL) Masanja Kadogosa amesema tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo mwezi wa Februali mwaka huu amefanikiwa kuliweka shirika hilo amelifanya liweze kufanya kazi kwa ushindani.

Amesema katika kipindi cha miezi mine ya uongozi wake amefanikiwa kuliwezesha shirika hilo kuongezeka kwa mapato toka  ya treni ya masafa marefu  toka mapato ya milioni 80 kwa mwezi hadi kufikia shilingi milioni 155 ambapo ongezeko hili ni sawa na asilimia 92.3.

Huku mapato ya treni inayofanya kazi ndani ya Jijini La Dar es salaam yameongezeka toka wastani wa milioni 1 kwa siku hadi kufikia milioni 3.3 ongezeko hilo ni sawa na asilimia 92.3.

Hata hivyo,amesema sababu iliyochangia mapato hayo kuongezeka imetokana na kuweka misingi mizuri rafiki kwa wateja jambo analodai limepelekea mapato hayo kuongezeka.

Mbali na Mapato hayo pia,Kagadosa amesema katika kipindi hicho kifupi alichukua nafasi hiyo toka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo,Elias Mshana amefanikiwa kufufua mabehewa 24 kwenye karakana  ya Reli iliyoko Dodoma huku juhudi za kufufua mengine zikizidi kuendelea.

Amefafanua kuwa hataa ya kufufu mabehewa yaliyokufa kunaokoa fedha ambazo zingekwenda kununu mabehewa hayo ambapo ufufuaji huo umeweza kuokoa Bilioni 5.52 kwa mabehewa hayo 24 endapo yangeenda kununuliwa.

Kagadosa amesema kwa sasa Kampuni yake imeweza kutatua malalamiko yaliyoyanatolewa kutoka kwa wafanyakazi wa TRL kwa hatua ya shirika hilo kuchelewa kupeleka michango ya mifuko ya jamii  pamoja na Bima ya Afya ambapo amedai kwa sasa wameanza kupelekea michango hiyo.


Hakuna maoni