RAIS MAGUFULI ABARIKI MIKUTANO YA UPINZANI KUPIGWA STOP,SOMA HAPO KUJUA
RAIS John Magufuli leo akiwa Ikulu, jijini Dar es
Salaam ameonesha kukerwa na mihadhara ya kisiasa nchini na kuhoji, “watu
watakula wapi?” anaandika Hamisi Mguta.
Kumekuwepo na mvutano kati ya
Jeshi la Polisi na vyama vya siasa hususan vya upinzani baada ya kutolewa
tangazo la kuzuiwa mikutano na maandamano ya kisiasa nchini.
Hatua
hiyo imesababisha kuibuka kwa mgogoro huku Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema pia mwenyekiti
mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akifungua kesi
mahakamani kuwashitaki baadhi ya viongozi akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali
.
Wakati
akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana kutoka Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), Rais Magufuli amesema, baada ya kufanyika uchaguzi
kinachofuata ni maendeleo.
Ameeleza
kuwa, kila nchi baada ya uchaguzi kuisha kinachofuata ni kutekeleza ahadi na
kwamba, haiwezekani muda wote iwe ni kufanya siasa.
Amehoji,
kama siasa ikifanyika kila siku watu watakula wapi? “Haiwezekani kila siku ni
siasa, watu watakula wapi?”
Hata
hivyo amesema, hayuko tayari kuona mtu yoyote katika utawala wake akichelewesha
safari yake ya mafanikio katika miaka yake mitano ya utawala.
Amesema,
serikali inayoongoza nchi sasa ni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na yapo
waliyoahidi katika kipindi cha miaka mitano ambayo anapaswa kuyatekeleza.
“Wanasiasa
wafanye sasa kwa ushindani wote, iwe madiwani wapeleke hoja ngumu kwa wananchi
au wawakikishi wa wananchi ili baada ya miaka mitano wananchi wahoji
tuliyoyatekeleza na kushindwa kuyatekeleza,” amesema.
Aidha,
amesema NEC imefanya kazi nzuri kusimamia uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba mwaka
jana na kwamba, taasisi hiyo imerahisishia kuendelea na majukumu yake vizuri.
Hata
hivyo ameieleza NEC kuwa, suala la ujenzi wa ofisi maalum ya tume lipo pale
pale kwa mapendekezo ya kwamba, ofisi hiyo ijengwe Dodoma ili kutimiza lengo la
Mwalimu Julius Nyerere la serikali kutoka kuhamia huko.
“Kama
mapendekezo yangu yatakubaliwa basi tutaweza hata kupunguza msongamano wa
foleni Dar es Salaam,” amesema.
Ujenzi
huo wa ofisi za NEC ni ule ulioelezwa kutekelezwa kupitia Sh. 12 bilioni ambazo
ilirudishwa na Damian Lubuva, Mwenyekiti wa NEC wiki chache zilizopita baada ya
fedha hizo kutotumika Uchaguzi Mkuu.
Amesema,
cheo cha rais ni msalaba aliotwikwa na wananchi lakini bado ushirikiano na
wanasiasa wenzake upo palepale.
“Ili
nchi isonge mbele, lazima kuiweka nchi na maendeleo ya watu kwanza kisha vyama
baadaye. Uongozi ni msalaba hivyo unahiyaji msaada wa Mungu,” amesema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni