KUBWA LEO,MADUDU YA KUTISHA BODI YA MIKOPO YA ELIMU,VIGOGO WAGAWANA VYAO,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
HAKIKA Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu Juu
nchini (HELB) ilikuwa inatafunwa kwa ufisadi ndivyo naweza kusema baada Wizara
ya elimu,Sayansi na Teknolojia kubaini madudu mazito ndani ya Bodi hiyo.
Madudu hayo ni kuwepo kwa wanafunzi hewa ambao
walikuwa wananufaika na mikopo hiyo.
Pia kuwepo na wanafunzi ambao walikuwa wananufaika
na mikopo hiyo kwa kulipwa na pande mbili yaani
upande wa Bara HELSB pamoja na Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB).
Sanjari na
hayo pia Bodi hiyo imebainika kutumia Kampuni za Kidalali katika kuwadai wanafunzi
mikopo huku ikiwa kinyume na taratibu za Bodi pamoja na Kampuni hizo kugubikwa na udanganyifu katika usajili wake kwenye
orodha ya Makupuni nchini (BRELA).
Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Waziri
Elimu,Sayansi na Teknolojia amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati
alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema baada ya terehe 16
Febreuari ya mwaka huu kuwasimaisha watendaji wa juu wa Bodi hiyo kutokana na
kutokekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika taasisi hiyo pamoja na kupisha
uchunguzi zaidi,
Ambapo Ukaguzi huo ulifanyika kwa kipindi maalum
hadi marchi 2016 ,katika uchunguzi huo profesa Ndalichako amesema kumebainika
kuwepo kwa wanafunzi hewa 50 ambao wamekuwa wakipata mkopo ambapo imeitia
hasara serikali mamilioni ya fedha.
Amesema Uchunguzi huo pia umebaini zaidi ya
wanafunzi 919 hewa ambao wanaelezwa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ambao walikuwa
wanapelekewa mikopo katika Chuo hicho ambapo kwa sasa imegundulikwa wanafunzi
hawasomi chuo hicho ambao wameitia hasara
serikali zaidi ya Bilioni Tatu.
Profesa Ndalichako amesema mbali na wanafunzi hao
hewa pia Uchunguzi huo umebaini kuwepo kwa wanafunzi zaidi ya Laki moja ambao
kisheria walikuwa wanatakiwa kuaza kulipa fedha walizokopesha na Bodi hiyo
kutokana na kipindi cha mwaka mmoja
kupita mara baada ya kumaliza chuo kama sheria inavyosema lakini amedai cha
kushangaza wanafunzi hao bado hawajaanza kulipa mikopo hiyo.
Amesema licha
kushindwa kukosanya Mikopo hiyo,Uchunguzi umebaini kuwa kuwepo na udhaifu mkubwa
katika mfumo wa utunzaji taarifa za marejesho ya mikopo.
Amefafanua kuwa Kumbukumbu za HESLB zinaonyesha
Madeni kwa kiwango pungufu kwa deni halisi huku akitoa mfano wanafunzi 262
walinufaika na mikopo kiasi cha SHS Bilioni 10 lakini amedai kuwa katika
kumbukumbu za Bodi hiyo wanatakiwa kurejesha Bilioni 5.5 ambayo inakuwa pungufu
ya karibia nusu ya deni ilo.
UFISADI KATIKA KAMPUNI ZA UDALALI ZILIPEWA TENDA
YA KUFUATILIA WADAIWA.
Profesa Ndalichako pia amesema Uchunguzi huo
umebainika kuwepo kwa utapeli anaoita wa “kitoto” kwa kampuni za udalali
zilizopewa kufuatilia tenda kwa madai kuw.
“Iweje leo bodi ya mkopo iwakopeshe wanafunzi hao na
kabla hata ya kutoa mikopo hiyo teyari ilichukua anuani zao,kuwafahamu wadhamini wao
kwenye mikopo hiyo,pamoja na kujua wanapotoka lakini cha kushangaza wakati wa
kudai fedha wanazitumia kampuni za udalali kudai fedha hizi”alishangaa Profesa
Ndalichako.
Amesema Kampuni hizo zimebainika kuwepo na
udanganyifu katika usajili wake huku akitaja jina Kampuni moja “Macho Mengi” ambayo haina hata usajili kwenye
orodha ya Makampuni huku Kampuni mojawapo ikiwa imesajili Brela kwa kazi ya
kufafirisha vifaa vya Jenzi jambo analodai inakuwa Kampuni ya Ujenzi inakuwaje leo ndio ipewa
tenda ya kukusanya madeni ya mikopo.
Baada ya Madudu hayo,Waziri ameipa wiki mbili Bodi
ya HESLB kuhakikisha wanawachukulia hatua kali za watumishi walihusika na
ufisadi huo.
Ikiwemo kupitia Dosari zilizojitokeza pamoja na
kuhakikisha wanavichukulia vyuo vikuu vilivyohusika kuwaruhusu wanafunzi
kuchukua mikipo wakati wanasomavyo viwili tofauti
MADUDU
YABAINIKA NACTE
Katika hatua
nyengine Waziri huyo pia ameeleza madudu ya kutisha ndani ya Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) kutokana na
watendaji wake kushindwa kusimamia vyuo 567 vya ufundi vilivyopo chini yake kwa
hatua ya kuwaruhusu wanafunzi “Vilaza” kujiunga na vyuo mbali mbali nchini.
Amesema Kamati Maalum iliyoundwa na yeye amesema
imebaini pia kwa NACTE kuhusika hata katika kuwadahili watu wanasomea Shahada
ya Kwanza (Bachelor) na Shahada ya Umahiri (Master) wakati sio jukumu lake
lilopo kisheria.
Ameeleza kuwa ndani ya Bodi hiyo kumegundulika
kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na sifa.
“Leo inakuwaje mtu mwenye shahada moja anawasimia
watu kama maprofesa huyu ataweza vipi”alihoji Profesa Ndalichako.
Profesa huyo amesema
Nacte wameshindwa hata kuhakiki
ubora wa vyuo vya kati nchini.
Hata hivyo,Profesa Ndalichako aliagiza Baraza hilo
kutatua Changomoto hizo haraka sana.
Maoni 2
Ndalichako ahsante sana kwa kulibaini hilo ombi langu kwako vyuo vingi hasa vya private havina vigezo lakini vimesajiriwa kisheria mfano kuna vyuo vinapeleka wanafunzi wenye D nne eti kusomea ufamasia, D moja kusomea komputa lkn ki msingi wanaotakiwa kusomae hizo kozi ni wenye ufauru angalau wa so pitdv3uo vyote ka vile vya cheti na deppitienivyotechetikwa utafiti ili mweze kuviadhibu kwa maana vingi havifuati vigezo mlivyotoa katika kudahiri wa watu wake.Elimi bila ukali kwa wanaoiharibu itaendelea kushuka thamani kama ya pesa.
Chapisha Maoni