BREAKING NEWS,TUNDU LISSU ANASAKWA NA JESHI LA POLISI,YALIYOMKUTA ZITTO KABWE NAYE YAMFUATA,SOMA HAPO KUJUA
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
linamsaka Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu kwa kile wanachodai mbunge
huyo ametomlea lugha chafu Rais John Magufuli.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Akithibitishwa kutafutwa kwake Lissu ambaye ni
Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameiambia
Fullhabari.blog kuwa Jeshi hilo limemtaka
ajisalimisha Makao mkuu ya polisi ya Kanda hiyo leo saa tano asubuhi, kutokana
na kutoa kauli ya kumuita Rais Magufuli ni “Dikteta uchwara” .
Lissuambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzania Bungeni alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kumaliza
kusikiliza kesi aliyofunguliwa na serikkali kwa kufanya Uchochezi kwenye Gazeti
la Mawio.
“Ni kweli natafutwa na jeshi la Polisi kutokana na
kutoa kauli yangu jana wakati nikuzungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kutokana mahakamani kwa kumuita Rais Magufuli ni Dikteta Uchwara,na nitakwenda
polisi hapo baadae saa tano asubuhi,nikasikiliza hicho wanachonitafutia”amesema
Lissu.
Lissu amesema kwa sasa Tanzania inaongozwa na
watawala wasiotaka kuambiwa ukweli huku akisema atambana nao mpaka haki ya
msingi ya wananchi itakampoheshimiwa.
“Sasa hivi nchi yetu ndio ilipofika,mtawala hataki
kuambiwa ukweli,hataki kukoselewa,badala ya kupambana na umasikini wa watanzania yeye anapambana na sisi wapinzani nakuhakikishia tutapambana naye mpaka haki ya
msingi itakaposikilizwa”ameongeza Lissu.
Kuitwa huku kwa Lissu kunakuja ikiwa ni wiki mbili kupita baada ya
Kiongozi mkuu wa Chama cha Act-Wazalendo,Zitto Kabwe kuitwa na Polisi kwa madai
naye kutoa lugha ya inayoitwa ya uchochezi.
Mbali na Zitto kuitwa huko Polisi pia kuna kuja ikiwa ni teyari
Rais Magufuli akiwa amepiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa pamoja na
maandamano mapaka 2020,
Huku wanaharakiti mbali mbali na wanasiasa wakiwa
wameibeza hatua hiyo kwa kusema Rais anavunja katiba aliyoiapa kuilinda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni