TUNDU LISSU AJILIPUA TENA MAHAKAMANI,ASEMA ANAMTAKA "DIKTETA UCHWARA" AJE MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) akiwasili mahakama ya Kisutu pamoja na wafuasi wa chama hicho
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki
amesema, ‘namtaka dikteta uchwara mahakamani,’anaandika Faki Sosi.
Lissu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
amesema hayo leo muda mfupi baada ya kutoka kusikiliza shauri lake katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam la kudaiwa kutoa kauli ya
uchochezi.
“Mimi na jopo
langu la mawakili tunamtaka niliyemuita diktekta uchwara aje mahakamani
kuthibitisha udikitekta uchwara wake,” amesema Lissu
.
Lissu
amefunguliwa shitaka la uchochezi katika mahakama hiyo, kesi yake inasikilizwa
na Hakimu Yohona Yongolo ambapo kwa upande wa mashitaka, unawakilishwa na
Benard Kongolo, wakili wa serikali mkuu.
Lissu
alijisalimisha jana 5 asubuhi katika kituo hicho cha polisi ambapo alizuiliwa
kupewa dhama na kulala hadi alipofikishwa mahakamani leo.
Wafuasi na
viongozi mbalimbali wa Chadema walifika mahakamani hapo akiwemo Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa chama hicho taifa; Salum Mwalim, Kaimu Katibu Mkuu Zanzibar na
Benson Kigaila, Mkuu wa Operesheni wa chama hicho.
Wakili Kongolo
amedai kuwa, Lissu alitenda kosa hilo tarehe 28 Juni mwaka huu katika eneo la
Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kuzungumza;
“Mamlaka ya
Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila
Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila
sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza
nene.’’
Hata hivyo,
Lissu amekana shitaka hilo, amedhaminiwa na wadhamini wawili waliosaini hati ya
Sh.2 milioni kila mmoja na masharti ya kutosafiri nje ya nchi na kwamba,
upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo itatajwa kwa kusikilizwa tarehe 2
Agosti mwaka huu.
Upande wa
utetezi kuliwakilishwa na mawakli 11 miongoni mwao ni Michael Ngolo, Peter
Kibatala, John Mallya, Hekima Mwasibu, Omari Msemo, Jeremia Mutasebya na
Juma Nasoro.
Nje ya Mahakama
Alipotoka nje ya
mahakama Lissu alizungumza na wafuasi wa Chadema walifurika katika viwanja
hivyo pamoja na waandishi wa habari ambapo amesema, “nilijua kwamba wenye
busara watanyamaza baada ya mimi kutoa kauli ile juzi mahakamani hapa.
Hata hivyo,
Lissu amesema kuwa, katika kituo alicholazwa ameshuhudia watu wakiteseka
kutokana na kutopelekwa mahakamani kwa muda wa wiki mbili hadi mwezi mmoja na
kuwa, hupewa mateso makali mpaka kusababisha wengine kuvunjwa miguu.
Mbowe amewaambia
waandishi wa habari kuwa, uonevu wa utawala wa sasa unafanywa bungeni na nje ya
bunge na kwamba, hawatakata tamaa ya kupigania haki.
Wakati huo huo
Jeshi la Polisi limewatia mbaroni wafuasi wanne wa Chadema walikuwa wamebeba
mabango yenye maneno ‘Dikitekta Uchwara nenda Burundi,’ Polisi ‘Uchwara acheni
kutumika’ na ‘Lisuu Tanzania inakuhitaji
Hakuna maoni
Chapisha Maoni