CUF YAMTAKA DKT.SAMIA KUSISITIZA UHURU NA HAKI UCHAGUZI MKUU 2025
Chama Cha Wananchi( CUF) kimemtaka Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchaguzi mkuu unaofanyika Mwaka 2025 uwe wa uhuru nawa haki ili kuendelea kulinda na kukuza Demokrasia Nchini.
Hatua hiyo ya CUF imetokana na kile ilichodai kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 ulikua hauna uhuru na haki kwa wagombea wa vyama vya upinzani kutokana na Demokrasia kusiginwa na TAMISEMI iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi huo.
Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 29,2024 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa tathmini ya baadhi ya mambo yaliyofanyika mwaka 2024 ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao amesema kuwa ulikua na dosari kubwa na kuharibu Demokrasia kwa ujumla.
Prof.Lipumba amesema kuwa uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2025 unapaswa kusimamiwa na tume huru ya Taifa ya uchaguzi( INEC) na sio TAMISEMI kama ilivyofanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa,huku akisisitiza kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anapaswa kusisitiza kuwepo kwa uhuru na haki katika uchaguzi huo.
"Tunamuomba Rais Samia asisitize kuwepo kwa uchaguzi wa uhuru nawa haki 2025,itafikia hatua wananchi uvumilivu utafikia kikomo na tutalitumbukiza Taifa letu kwenye machafuko " amesema Prof Lipumba
Nakuongeza kuwa "tukubali Rais Dkt.Samia ameteleza kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,ajaribu kurekebisha mambo kwenye kwenye uchaguzi mkuu na iwepo tume huru ya Taifa ya uchaguzi ili itekeleze majukumu yake kwa uhuru nakwa haki.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vitongoji na Vijiji umefanyika Novemba 27,2024 ,na umeonekana kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kusambaa kwa karatasi bandia za kupigia kura,pia baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani kuenguliwa majina yao kwenye daftari la mpiga kura kwa sababu zisizo za msingi,hali ambayo imeelezwa iliipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 90, kufuatia mtokeo ya jumla yaliyotangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa Novemba 29,2024.
Katika hatua nyingine Profesa Lipumba ameishauri Serikali kuhakikisha inawekeza kwa tija katika sekta ya Elimu,Afya na Rasilimari watu ili kuhakikisha Taifa lina vizazi vyenye Elimu bora,Afya bora na Uchumi imara nakua na maendeleo endelevu kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Profesa huyo wa uchumi ametumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wote heri ya Mwaka mpya wa 2025 wenye mafanikio lukuki na kuweza Kutekeleza ipasavyo malengo yao waliyojiwekea.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni