WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WAISOMA NAMBA SASA,BAADA YA UDOM NGOMA YAAMIA UDSM,SOMA HAPO KUJUA
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika mgomo |
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
wamegoma kusitisha mgomo wao mpaka pale pesa za kujikimu zitakapoingizwa kwenye
akaunti zao, anaandika
Faki Sosi.
Mgomo huo umeanzishwa baada ya
kucheleweshwa fedha zao za kujikimu zinazotolewa kila baada ya siku 60.
Wanafunzi
hao wanadai fedha hizo baada ya kupita siku tano bila kupewa taarifa yoyote
ikiwemo kwamba, serikali haina fedha.
Mgomo
huo umeanza saa mbili asubuhi ambapo mpaka sasa haujakoma kutokana na msimamo
wa wanafunzi hao wa kutoacha kugoma mpaka watakapopatiwa haki yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari Prof. Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa UDSM amesema
kuwa, fedha hizo zitatolewa kabla ya kufuka Saa 12 jioni.
Awali
msimo wa wasomi hao ni kumtaka Paul Makonda, Mkuu wa Dar es Salaam, Ally Salum
Sapi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya
Kinondoni kuzungumza nao.
Erasmi
Leon, Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDSM na Mshangama Shamira,
makamu wake wamesema kuwa, mgomo husika utaendelea mpaka pale
watakapothibitisha kuwa, fedha zao zimeingia katika akaunti zao.
Wanafunzi
wamekusanyika katika eneo la Revolution Square lililopo chuoni hapo kwa amani
huku wakiimba nyimbo mbalimbali za uzalendo.
“Kama
sio juhudi zako Nyerere…, Sitasimama maovu yakitawala…., Vijana tusilale bado
mapambano…. alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka….”
Wamesikika wakiimba.
Hata
hivyo, mpaka muda huu viongozi waliowahitaji kuzungumza nao hawajafika kwenye
eneo la tukio.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni