SAKATA LA MAUAJI YA FAMILIYA BILIONEA MSUYA,KAMANDA SIRRO AMDAKA HUYU,SOMA HAPO KUJUA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikiria mtu mmoja kwa
tuhuma za mauaji ya Anneth Msuya aliyeuawa kwa kuchinjwa hivi karibuni,
Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa
wanamshikilia mtu huyo kwa uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya mwanamke
huyo.
Sirro
amesema kuwa katika tukio la mauji ya mwanamke Anneth Msuya polisi wako
katika upelelezi na hawezi kutaja jina la mtu wanayemshikilia kutokana
na sababu za kiusalama na kuhofea kushindwa kuwakamata watu wengine.
Tukio
la kuuawa kwa Anneth Msuya lilitokea Mei 26 nyumbani kwake Kibada,
Kigamboni jijini Dar es Salaam, limekuwa ni mwendelezo wa matukio
mengine ya uhalifu kwa familia yao yaliyowahi kutokea baada ya kifo cha
kaka yake, Msuya aliyeuawa Agosti 2012 kwa kupigwa risasi, tukio
lililofanyika mkoani Kilimanjaro.
Wakati
huo huo majambazi wawili wameuawa kwa kupigwa na polisi na mmoja
aliuawa wananchi baada ya bastola yake kuishiwa risasi huko maeneo ya
Mburahati Minazini akiwa anawatupia risasi, huku mmoja akikamatwa akiwa
na pikipiki aina ya boxer yenye namba za usajili MC 444 BFY na wananchi
walimshambulia.
Bunduki
waliokuwa nazo ni bastola yenye namba za usajili 649440 na bastola
nyingine aina ya Chinese Star ambazo silaha hizo ndizo walikuwa
wanafanyia uhalifu.
Amesema
pia jeshi la polisi linaendelea na operesheni mbalimbali na wanapata
ushirikiano na wananchi ikiwa ni pamoja na kukamata watoto wadogo
wanaotembea kundi kubwa na kuvamia na kupora kwa wananchi (maarufu panya
road)
Pia
alimalizia kwa kusema, Jeshi la polisi limekusanya sh. 548, 160,000
kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabara kwa magari na
pikipiki.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon
Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) juu ya Jeshi
lake kuendelea na operesheni mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon
Sirro akionyesha silaha mbili aina ya bastola, zilizokamatwa katika
Matukio ya Uhalifu jijini Dar leo.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon
Sirro akionesha gari iliyo tumika kufanya uhalifu leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina (CP), Simon Sirro
akionesha silaha mbalimbali zinazo tumika kufanyia uhalifu (Picha na
Emmanuel Massaka Globu ya Ja Jamii)
Hakuna maoni
Chapisha Maoni