UKAWA WAMALIZANA NA MKURUGENZI WA ILALA,SASA WAMACHINGA WATAKIWA KUONDOKA HARAKA SANA,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meya wa Manispaa ya Ilala,Charles Kuyeko akizungumza na Waandishi wa habari |
HATIMAYE mgogoro uliopo kati ya
Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Isaya
Mnguruni kuhusu hatua ya kuwahamishwa
wafanyabiashara ndondogo wanaofanya kazi maeneo ya karikoo,mgogoro huo umefikia
tamati.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Baada ya Madiwani hao na
mkurugenzi huyo kukubalina kutatua changomoto za masoko ya wafanyabisha hao
ambao wanatakiwa kwenda huko.
Awali Mngurumi aliwataka
wafanyabishara hao kuondoka kwenye maeneo ya katikakati ya jiji na kuwataka
kuelekea masoko ya Pugu,Kivuli,Kigogofresh,Ukonga na Tabata jijini hapa,ambapo mara baada
mkurugenzi huyo kusema hivyo-
Ndipo likaibuka Baraza la Madiwani
ambalo kwa kiasi kikubwa linaongozwa na Vyama vya Upinzani kupinga hatua ya
wafanyabishara hao kuhama kwa kile wanachokidai kuwa maneohayo wanayokwenda
yanachangamoto za maji,umeme,Barabara na huduma za choo,ambazo zitawakwamisha
wafanyabishara hao.
Akizungumza na waandishi wa Habari
leo Jijini hapa,Meya wa Manispaa ya Ilala,Charles Kuyeko amesema madiwani kwa
kauli moja wamelidhia hatua ya Mkurugenzi huyo mara baada ya kuhaidi kutatua
changamoto ambazo zilizowafanya wapinga hapo awali.
“Tumekubaliana na Mkurugenzi,baada
ya viongozi wa Halmashauri kukubaliana na sisi kutatua changomoto za Barabara
kuelekea kwenye masoko hayo,pia wameshaweka huduma ya umeme ambayo mwanzo
ilikuwa haipo kwenye masoko hayo,lakini tumeona wameweka huduma ya vyoo lakini
haijakamilika,”amesema Kuyeko.
Kuyeko amesema Baraza la Madiwani
alikupinga hatua ya wafanyabishara kwenda huku bali walikuwa wanataka
kujilidhisha uwepo wa miundombinu rafiki
itakayowasaidia wafanyabishara,
Amesema Wafanyabishara wanatakiwa
kuondoka kwenye maeneo hayo haraka ili kupisha mradi wa Mabasi ya mwendo wa
haraka (DART)ambayo yanatarijia kuanza haraka hivi karibuni.
“Kwa mfano maeneo ya Kariakoo ambapo
wafanyabisha hawa wanafanya shughuli zao, kuna mradi wa mabasi haya
unaanza,kwahiyo nataka watii tu agizo hili,na waende kwenye maeneo tuliowambia
kwani mradi huu ukianza lazima tu wanatakiwa kuondoka”amesema Kuyeko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo,Mngurumi amewapongeza madiwani hao kuungana kwa pamoja katika
masuala ya maendeleo huku akiwahadi kutatua changomoto zilizobakia ambao zilikuwa
zinatakiwa na madiwani hao.
Amewataka Wafanyabishara kutii agizo
hilo,na kwenda kwenye maeneo hayo aliyotajwa,
Hata hivyo amesema Halmashauri yake
haitasita kutumia nguvu kwa wafanyabiahara ambao watakaidi agizo hilo
Hakuna maoni
Chapisha Maoni