Zinazobamba

TRA YATANGAZA KUFIKIA MALENGO YAKE,YAANZA KUWAPIGA MSASA WATUMISHI WAKE,SOMA HAPO KUJUA



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4MZfBN90Y6IjYRujnZzVoOsG303Uk8x6tcc1evy4dFSVoV6Ho0eDsX14sbi7QHeOxarVoa83V6-ST9aawKbJ6xEaKCRPvAAK9n9AxegG7Nng_vLySF5TR7Z0MPj6D1UJq4_5PbpuGXlhb/s1600/DSCF0036.jpg




KamishinaMkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata Akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam,
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhONL6J0Wwgak68MLx3xHje4DaS2FWC__AFP5xbmgkaHvlsRCqsj456mt96bM0pbFph-e4dKytwt9_30IdHwyYuXhFBVRB7xZw07kjDvCKWCbET2-p26wg8yyx-oLbSJMx2Gk5K74a0_KUy/s1600/DSCF0022.jpg

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Kodi Prof. Isaya Jairo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA.



IMEELEZWA kuwa Mamlaka   ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwakawa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.

Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata  ameeleza hayo wakati akifungua  hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo  

Kidata amesema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha  sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.

“Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. Kidata.

Aidha Bw. Kidata amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa  kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka mmoja yanayoendana na usaili mpya kwa wahitimu ili  kufanya Mamlaka hiyo kuwa na
wafanyakazi waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.
Naye pia, Mkuu wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo alisema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha mungu katika kazi zao.








Aidha Kaimu Mkurugenzi
Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro aliwataka wafanyakazi wote
wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo
hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo
ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.

Hakuna maoni