SERIKALI YA MAGUFULI YAWAKUZA WAPINZANI,SOMA HAPO KUJUA
HATUA ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa
moja ya imetajwa kuathiri zaidi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuliko vyama vya
upinzani, Anaandika
Pendo Omary.
Wakizungumza na chanzo changu wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamesema,
hatua hiyo inachangia kuwajenga wabunge wa upinzani ambao sasa taarifa zao
zinafika zaidi kwa wananchi kuliko za wabunge wa CCM.
“Ni
wazi serikali na CCM wanashirikiana kudhibiti bunge lisirushwe ‘live’ wakiwa na
lengo la kuwakomoa wapinzani. Wabunge wa CCM nao wanafurahia hatua hii.
“Wananshidwa
kujua wao wenyewe wanajinyimwa fursa wananchi kuona mambo mazuri yanayosemwa
bungeni na mawaziri wao,” amesema Khamis Rajabu, Mkazi Kariakoo.
Grace
Lameck, Mkazi wa Mwananyamala amesema, “Sasa tunaelewa kwa nini bunge linazuiwa
kurushwa ‘live’, ni kuficha udhaifu wa wabunge wa CCM.
“Mfano
ni hili sakata la Goodluck
Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) hivi karibuni kudai kwamba, anayeteuliwa kuwa
mbunge wa viti maalum ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
lazima aitwe ‘beby’ ikiwa na maana ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi. Huku ni
kufilisika hoja,” amesema Grace.
Grace
amesema tarehe 13 Mai, 2016 baada ya Nape Nnauye ambaye ni Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na
matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 Mlinga alisema “ingekuwa amri yangu
tungechonga sanamu la Diamond tukaliweka kwenye mnara wa Askari, ule mnara
tumeuchoka.”
Na
kwamba, kauli hiyo imechangia wanachi kukosa imani na uteteuzi wa wabunge wa
CCM kuhusu kutorushwa bunge moja kwa moja.
Akiandika
katika ukurasa wake wa Facebook, Irene Kiria, Mkazi wa Dar es Salaam anasema
“bado sijaelewa kwa nini Bunge limeamua kuwapa upinzani umaarufu kiasi hiki.
Social media (mitandao ya kijamii) imetaja zaidi yanayosemwa au kufanywa na
wabunge wa upinzani kuliko wa CCM lakini mabaya ya CCM kuliko ya wapinzani.
“Kwa
utendaji wa Rais Magufuli ulivyokubalika, wengi wetu tulipata mashaka iwapo
upinzani utakuwa na nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano. Binafsi nikiri
sasa kwamba, nilikuwa miongoni mwa waliojiuliza hivyo, kumbe nilikosea,”
ameandika Kiria.
Pia
Kiria ameanndika “kuzuia bunge ‘live’ ni ushahidi kwamba kimwili tunaishi
katika karne ya leo lakini fikra na matendo yetu bado yako karne iliyopita.
Matokeo ni huu mkanganyiko tunaoshuhudia, kulifanya jambo kusambaa na
kufahamika zaidi kwa kitendo cha kujaribu kulizuia.
“Nadhani
serikali na CCM wanatakiwa kutathmini namna wanavyoathirika kwa kufuta bunge
‘live’ isipokuwa kama hilo ndilo lengo lenyewe – kuwafanya wapinzani wang’are
zaidi.”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni