MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA MSIKITINI NCHINI ,HALI YAANZA KUWA MBAYA,SOMA HAPO KUJUA
NDANI ya Msikiti wa Rahma ‘Masjid Rahma’ mkoani
Mwanza mauaji yametokea, watu watatu waumini wa msikiti huo wamepoteza maisha, anaandika Moses Mseti.
Watatu wakiwa wamepoteza maisha
huku mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya. Tukio hilo limetokea jana kwenye msikiti
huo uliopo Ibanda Relini, Mtaa wa Utemini katika Kata ya Mkolani wilayani
Nyamagana. Watu hao waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na kundi la watu zaidi
ya 15.
Watu
waliouawa katika tukio hilo ni Ferouz Elias, Imamu wa msikiti huo, Mbwana Rajab
na Khamis Mponda ambaye ni dereva bodaboda. Aliejeruhiwa ni Ismail Abeid,
mwanafunzi wa Shule ya Kiislam ya Jabar iliopo Nyasaka jijini humo.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 2:30 usiku wakati waumini wa msikiti
huo wakiendelea na Swala ya Isha.
Wakati
swala hiyo ikiendelea, ghafla kundi hilo la watu waliingia msikitini hapo na
kuanza kuhoji “kwanini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiriwa na
polisi” kauli ambayo ilifuatana na mashambulizi hao.
Mashuhuda
wa tukio hilo ambao hawakutaka kutajwa majina yao (yamehifadhiwa) wamesema
kuwa, yawezekana chanzo cha mauaji hayo kinatokana na kuwepo kwa misikiti
miwili ambayo ina uhasama wa muda mrefu.
Shuhuda
moja amesema, “unajua katika eneo hili kuna msikiti miwili (anaionesha). Hawa
kwa muda mrefu wapo katika uhasama sasa hili ndilo linaweza kuwa tatizo.
“Misikiti
hii kama unavyoona ipo katika pori na ipo nje ya jiji na wakati wanatekeleza
mauaji hayo, suala hili linatupatia wasiwasi mkubwa sana,” amesema.
Shuhuda
huyo amesema, wauaji hao walikuwa na silaha za moto aina ya SMG pamoja na
mabomu ya moto ya kutengeneza na kwamba, walirusha mabomu hayo lakini
hayakuleta madhara yoyote.
Shekh
Hussein Ibrahim, Mwenyekiti wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)
Wilaya ya Nyamagana amelaani kitendo hicho.
Amesema,
vitendo vya namna hiyo havikubaliki katika Dini ya Kiislam na kwamba, Waislam
wote wanapaswa kulaani matukio ya namna hiyo.
“Nilipata
taarifa saa tatu usiku na niliondoka na nilipofika eneo la tukio nilikutana na
watu watatu waliokuwa wamejeruhiwa na watu waliokuwa wamekufa tuliwachukua na
kuwapereka Bugando (Hospitali ya Rufaa ya Bugando) kwa ajili ya kuifanyia
uchunguzi zaidi,” amesema Shekh Hussein.
Amesema
kuwa, kufuatia tukio hilo Bakwata wameanza kuandaa mpango wa kuzuia na
kudhibiti matatizo hayo katika maeneo yao (misikitini).
Ahmed
Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (Sacp)
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema
kwamba, katika tukio hilo watu watatu wanashikiliwa na polisi mkoani humo kwa
ajili ya mahojiano.
“Polisi
hivi sasa tunaendelea na upelelezi wa tukio hilo na ninawaomba wananchi wawe
watulivu katika kipindi hiki, polisi tunaendelea kuchunguza na pindi
tutakapomaliza tutatoa taarifa kamili,” amesema Msangi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni