RAIS MAGUFULI AZIDI NG'ANG'ANIWA,UKIMYA WAKE KWA LUGUMI WACHUKUA SURA MPYA,YAFANANISHWA YA JK KWA KAGODA,SOMA HAPO KUJUA
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kimeeleza kuamini kwamba, Rais John Magufuli anayo siri ya Kampuni ya Lugumu na
INFOSYS hivyo anapatwa kigugumizi kuchukua hatua,anaandika Happiness Lidwino.
Pia chama hicho kimeeleza kwamba, ni
vema Rais Magufuli ajitokeza hadharani na kuwaeleza wananchi uhusiano wake na
Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye kampuni yake
ndiyo iliyofunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole katika Jeshi la Polisi
nchini.
“Chama kina mashaka juu ya mahusiano yao kwani licha
ya Kitwanga kutajwa mara kadhaa kuwa anahusika na mkataba tata wa Bilioni 37
kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
“Lakini bado ameziba masikio. Hivyo, akiendelea kuwa
kimya serikali yake itaangushwa kupitia waziri mkuu wake,” Salim Mwalimu, Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake
Mwalimu amesema, inawezekana Rais Magufuli anamasirahi binafsi na kampuni hiyo
na hivyo kushikwa na kigugumizi jinsi ya kutoa maamuzi.
“Ni kitu cha kushangaza sana kwamba hadi sasa bado
hajatoa kauli yoyote. Yeye ni mtaalamu wa kutumbua majipu kwa kupata habari
mitandaoni na kwa kusikia tu kama alivyofanya kwa Mkurugenzi wa Jiji lakini
majipu yaliyokaribu yake anayaogopa,” amesema na kuongeza;
“Tunamashaka na utumbuaji majipu wake inawezekana
anafanya hivyo kwa kulipiza kisasi na kuharibu urafiki wa marais waliopita, ama
anajifanya kutumbua watu ili awaweke watu wake waliokuwa wakimsapoti kwenye
kampeni.
“Kama kweli anafanya hakim bona majibu yanayomuhusu
hayatumbui?” amehoji Mwalimu.
Mwalimu pia amemtaka Waziri Kitwanga ambaye anatajwa
kuwa ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni yaINFOSYS iliyotumika kufunga mashine
za kuchukua alama za vidole (AFIS) , ajitokeze kujibu tuhuma hizo ama ama
ajiuzulu kwa kuwa hana sifa za kuwa Waziri tena.
“Kama bado wanafichiana siri yeye na rafiki yake
basi aige mfano kwa Edward Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye alijiuzulu kwa
kumstahi rafiki yake aliyekuwa akinuka usifisadi Rais Jakaya Kikwete. Kitwanga
ajipime na ajitafakari na kujitoa kwenye uwaziri,” amesema Mwalimu.
Awali, zabuni ya mkataba huo ilitangazwa tarehe 22
Septemba 2011 na kusainiwa terehe 23 Septemba mwaka huo huo ndani ya siku moja
mkataba ukasainiwa jambo ambalo ni hatari.
Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd ilipewa tenda na
Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika
vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh 37 bilioni.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 tu vya polisi ambapo tayari kampuni hiyo imelipwa Sh. 34 bilioni ikiwa ni asilimia 99 ya fedha za mkataba huo.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo 14 tu vya polisi ambapo tayari kampuni hiyo imelipwa Sh. 34 bilioni ikiwa ni asilimia 99 ya fedha za mkataba huo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni