Zinazobamba

TCRA YAVIPIGA PINI VITUO VYA EATV NA REDIO YA E.FM,NI MWENDELEZO WAKE SOMA HAPO KUJUA




MAMLAKA Ya Mawasiliano nchini (TCRA) imevitoza faini vituo viwili vya Utangazaji ambavyo ni Entertment Fm (E.FM) faini ya Milioni 4 pamoja na kituo cha Luninga cha East African Television (EATV) faini ya milioni 3 baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Akisoma hukumu hiyo mda huu Makao Makuu ya (TCRA)  yaliopo Jijini Dar es Salaam,Kaimu mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka hiyo,Joseph Mapumba amesema vituo hivyo vimekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 baada ya kufanya makosa ya udhalilishaji kwa  wanawake pamoja na kuchochea imani za ushirikina.

Mapunda ametaja makosa ya vituo hivyo, amesema mnamo tarehe 16/5/2016 kituo cha EATV katika kipindi cha muziki ambacho kilirusha majira ya saa 9.30 usiku kipindi hicho kilicheza Wimbo wa  panya ambao umeimbwa na msanii Blacketi ambaye amemshirikisha  Msanii Tecno.
Amesema Wimbo huo ulikuwa unamaudhui ya kumdhalilisha mwanamke kutokana na video hiyo kumwonyesha mwanamke akiwa “uchi” yaani hana nguo. Kwa kuvaa vazi la ufukweni huku akiwa hana nguo.
Amesema kituo hicho kilitenda kosa la kuonyesha video hiyo mda ambao bado watoto wapo macho jambo analosema  linakwenda na kinyume na sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 inayotaka vipindi vya aina hiyo kuwekea mda maalum yaani wa usiku.
Amesema mara baada ya Kamati hiyo kubaini makosa hayo waliwasiliana na uongozi wa EATV ambapo mkurugenzi wake,Regilna Mengi  alitoa utetezi wake kwa kusema video hiyo ilikuwa haina makosa kwani vazi ambalo mamlaka hiyo wanalosema lilikuwa ni kumfedhesha mwanamke ni vazi ambalo linavaliwa ufukweni huku akisemwa hapa nchini hakuna sheria inatoa mwongozo wa vazi gani livaliwa kwenye ufukwe.
Amesema mara baada ya kusikiliza utetezi ndipo kamati imeamua kituo hicho kupewa onyo kali kutokana na kukiuka kanuniza za utangaji ya mwaka 2005 pamoja na kuambiwa walipa faini ya milioni 3.
     KOSA LA REDIO YA E.FM.
Mapunda pia ametaja makosa yaliyofanya na E.FM redio,ambapo redio hiyo ilikiuka sheria hizo katika kipindi cha Ubaoni kinachorushwa kwaanzia saa 10 jioni hadi saa 1.00 ,ambapo amesema kipindi hicho cha tarehe 13/4/2016 ,mtangazaji wa kipindi hicho, alifanya mahojiano na binti ambaye alijitamburusha kuwa amefanya mauaji kwa kutumia imani za kishirikina.
Mapunda amesema binti huyo alisema amefanya ushirikina kwa kumuua mototo wa bosi wake huku akidai kuwa amesaidiwa na bibi yake.
Amesema kipindi hicho iimekiuka sheria ya utangazaji kwa hatua yake anayodai inachochea watu  kujiingiza kwenye imani za kishirikina.
Amesema mara baada ya kubaini kosa hilo,Kamati yake iliwasiliana na wamiliki wa Redio hiyo ambayo katika utetezi wake uliwasilishwa na Mhariri mkuu wa E.FM,Scholastika Mazula ambaye alisema katika kipindi hicho  hakulioni kosa  bali kipindi hicho kilikuwa na lengo ya kueleza ubaya wa imani za kishirikna kwa jamii.
Mapunda amesema mara baada ya Kamtai hiyo kusikiliza utetezi huo,ndio wakabaini kituo hicho kilikiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 inayokataza kurusha vipindi vitakavyohalibu  umoja na mshikamo wa taifa.
Amesema Kamati hiyo imetoa hukumu ya kupiga faini ya Milioni 4 pamoja na kuipa onyo kali ambapo endapo kituo hicho kikikaidi basi hawatasita kuichukulia hatua kali.

Hakuna maoni