CCM YAPIGWA MWELEKA NA CHADEMA,MAHAKAMA YAKATAA HUJUMA ZAO,SOMA HAPO KUJUA
PATRICK Asenga Diwani wa Kata ya Tabata (Chadema)
ameshinda kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Sudi Kasim aliyekuwa mgombea wa
kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, anaandika Faki Sosi.
Kasim alifungua kesi hiyo
akipinga matokeo ya kiti hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana kwa
madai kwamba haukuwa huru na haki.
Akitoa
hukumu ya kesi hiyo leo katika Mahakama hiyo, Frank Moshi hakimu aliyekuwa
akisikiliza shauri hilo amesema, anatupilia mbali kesi hiyo kwasababu mdai
ameshindwa kuthibitisha malalamiko yake.
Miongoni
mwa vitu alivyoshindwa kuthibitisha ni pamoja na uwepo wa vurugu katika kituo
cha majumuisho ya kuhesabia kura ambapo hata wakala wake ameshindwa
kuthibitisha hilo katika ushahidi wake.
Kutokana
na hali hiyo, hakimu alisema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki na kwamba
Asenga ni diwani halali wa kata ya Tabata na atalipwa gharama ya 30 milioni
kama fidia ya kesi hiyo.
Akizungumza
nje ya mahakama, diwani Asenga amewashukuru wananchi wake kwa ushirikiano
waliouonesha na kuahidi kuwa gharama za kesi atakazolipwa ataziingiza katika
miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Amesema
kuwa gharama hizo nakwamba atawasilisha madai ya fedha hizo mapema
ili aweze kulipwa.
“Nashukuru
wananchi wangu kwani nipo pamoja nao,mahakama imetenda haki.Hii kesi
ilinipotezea muda wa kuwatumikia ,lakini kwasasa nipo huru na nipo tayari
kuchapa kazi “amesema
Katika
kesi hiyo,wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ilala.
Katika
kesi hiyo, Kasim aliiomba mahakama hiyo itenguwe matokeo ya uchaguzi kutokana
na dosari mbalimbali zilizojitokeza na kwamba imtangaze yeye kama mshindi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni