PROFESA LIPUMBA AUMBUKA RASMI,RAIS MAGUFULI AMWACHA "SOLEMBA",SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)Profesa
Ibrahimu Lipumba ni kama ndoto yake imefutika ya kuwa mshauri wa uchumi wa
Utawala wa Rais John Magufuli baada ya Rais huyo kumteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa mshauri wa
Rais masuala ya uchumi.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa ya Ikulu kwa Vyombo vya habari inasema
Profesa Rurasitara ameteuliwa kushika nafasi hiyo,ambaye kabla ya kuteuliwa
nafasi hiyo alikuwa mhadhili wa kitivo cha uchumi kutoka Chuo kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM).
Kuteliwa kwa msomi huyo wa uchumi,kunazidi mwacha “solemba”Profesa
Lipumba ambaye alijiaminisha mara baada ya kujiuzulu nafasi ya uenyekiti mwaka
jana wakati wa kipindi cha Kampeni kwa kile alichokiita ni kutoridhika kwa ujio
wa Lowassa kugombania Urais kupitia vyama vinavyounda UKAWA.
Profesa Lipumba ambaye mara kuikacha nafasi hiyo
ilisemekana kuwa sababu ya kuachia nafasi hiyo ilitokana na kuhadiwa nafasi ya
ushauri wa uchumi kwa serikali ya aliyekuwa mgombea wa Urais wa Chama cha
Mapinduzi CCM ambaye sasa ni Rais, ili kuudhofisha upinzani.
Akizungumza kwa kujiamini Kigogo Mwandamizi kutoka
chama cha CUF ambaye alikataa jina lake kutajwa kwenye mtandao huu alisema
kutoteuliwa kwa Lipumba kwenye nafasi hiyo itakuwa ni fundisho kwa wanasiasa
mandumilakuili.
“Ninachokwambia huyo bwana (Lipumba) alichofanyiwa
itakuwa itakuwa fundisho kwa wanharakati wengene waoaaacha kutetea mabadiliko
kisa kuahidiwa vitu hewa,nazani amejifunza acha yamkute”amesema kigogo huyo.
Mbali na Mshauri huyo wa Uchumi,pia Rais Magufuli
amemteau Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Gerson Mdemu
kushika nafasi hiyo ambayo hapo awali ilishikwa na Apson Tulia ambaye sasa ni
Naibu spika wa Bunge l;a Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Maoni 1
Nonesense
Chapisha Maoni