SHEIKH JALALA AWATAKA WAISLAMU KUWEKEZA KATIKA TAFITI
![]() |
Sehemu ya Waislamu waliohudhulia uzinduzi wa Maktaba mpya kabisa Jijini Daresalaam Wakimsikiliza Sheikh Jalala akifafanua kuhusu umuhimu wa kusoma na kufanya Tafiti. |
Hapa Sheikh Jalala akizindua maktaba hiyo mpya. Maktaba hiyo inatarajiwa kuwahudumia Watanzania wote wenye malengo ya kujifunza zaidi elimu ya dini. |
Kiongozi Mkuu wa Chuo cha
Kiislam (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) Sheikh Hemed Jalala ameitaka jamii ya Kiislamu
kuwekeza katika tafiti kwani kufanya hivyo kutasaidia kufahamu mambo mengi
katika ulimwengu wa sasa.
Akizungumza katika uzinduzi wa
maktaba ya Maarifa Jijini Daresalaam,
Sheikh Jalala amesema njia pekee ya kuifahamu jamii na kuweza kufikisha ujumbe
wa Mungu kwao ni kufanya Tafiti.
Sheikh Jalala amesema ni wakati
sasa Masheikh na wanazuoni kuona umuhimu wa kuwekeza katika Elimu hususani
sekta ya Tafiti ili kuweza kwenda sambamba na karne ya sasa.
Akizungumzia umuhimu wa kufanya
Tafiti, Sheikh amesema Toka enzi hizo suala la Tafiti lilikuwa linafanywa na
Waislamu lakini miaka ya hivi karibuni dhima hiyo imekuwa kama imepokwa kwani
suala la tafiti limekuwa likifanywa Zaidi na Wazungu.
Akizungumzia umuhimu wa Masheikh
wa hapa nchini kufanya Tafiti, Sheikh Jalala amesema kuna umuhimu mkubwa kwa
Masheikh wetu kujikita katika kufanya Tafiti kwani kutasaidia kutambua changamoto
zinazoikabili jamii.
Amesema Masheikh wakifanya
Tafiti na kuja na maandiko mbalimbali kama vile Vitabu na Makala katika
magazeti mbalimbali itasaidia kuleta athari katika jamii na hivyo kusaidia
kuisukuma dini ya Uislamu mbele.
“Niwaombe Masheikh wenzangu na vijana kujituma
na kusoma kwa bidii ili kuisaidia jamii yetu, lazima tujenge utamaduni wa
kufanya tafiti ili ziweze kuwasaidia huko mbele ya safari” Alisema
Aidha katika
hatua nyingine, Wafuasi wa Shia Ithnasheriya Tanzania wametumia nafasi ya
ufunguzi wa Makataba hiyo mpya kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Imam Mah’d
(a.t.f.s) ambaye ni Kiongozi wa 12 baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) anayetarajiwa
kurudi tena duniani hapo baadae na kuleta Amani na Maelewano kwa watu.
Sheikh Jalala amesema Waislam
wote Duniani wanaamini ya kwamba Dunia hawezi Kumalizika mpaka aje mtu, mtu
huyo atakapo kuja atawaokoa wanadamu, kwenye matatizo na dunia ataibadilisha
kuwa kisiwa cha amani, Maelewano, Mshikamano na kuhakikisha dhuma na Ufisadi
unasambaratika duniani.
“Shaabn 15 siku kama ya leo (Jana)
mwaka 255 Hijiria alizaliwa Imamu wa 12 wa watu wa nyumba ya Mtume (saw). Jina
lake kamili ni Muhamad, lakini majina yake mengine ni Mahdi, Sahib uz Zaman.
Al-Hujjah, baba yake alikuwa Imamu wa 11 Imam Hassan al-Askari (as) na Mama
yake alikuwa Nargis Khatoon” hivyo Leo tunasheherekea hilo.
Suala la Itikadi ya Imam mahd limekuwa likizua
utata mkubwa sana baina ya Madhehebu ya waislamu duniani”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni