MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ALIPULIWA,CHAMA CHA ADC CHAMJIA JUU,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni
Naibu katibu mkuu wa chama cha
ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE ADC Ndugu DOYO HASSAN DOYO akionyesha baadhi ya
nyaraka mbalimbali ambazo zinaonyesha jinsi msajili wa Vyama vya siasa
alivyokiuka katiba ya chama hicho katika maelekezo yake ya kutaka mwenyekiti wa
chama hicho arejeshwe madarakani baada ya kutimuliwa na Bodi ya wadhamini ya
chama hicho
|
CHAMA cha Alliance for Democratic Chance (ADC)
kimemtaka msajili wa Vyama vya siasa nchini,Jaji Francis Mtungi kuacha
kupandikiza migogoro ndani ya chama hicho.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Hatua ya Chama cha ADC kufikia hatua hiyo imetokana
na Ofisi ya Msajili kuendelea kuutambua
uongozi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Said Miraaj Abdulla,ambapo
uongozi huo uliosimamishwa na chama hicho kutokana na kile kinachodaiwa kuwa amekiuka
kanuni za chama.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam,Naibu Katibu mkuu wa ADC Bara ,Doyo Hassani Doyo amesema chama hicho tarehe 27/4/2016 kilipokea
barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa inayo utambua uongozi
uliosimamishwa.
Amesema baada ya chama hicho kupokea barua hiyo
walibaini barua hiyo imekuwa na upungufu mkubwa na kuishusha hadhi ofisi ya
msajili.
Wanahabari wakiwa kazini |
“Barua hiyo ya msajili haikuzingatia matakwa ya
katiba yetu ya ADC,zaidi ya kubabea
ushabiki wa msajili na ishara ya wazi na kutaka kuendeleza mgogoro ambao teyari tulishaupatia ufumbuzi,lakini
msajili hana hoja zenye msingi tena inaonekana anamaslahi na uongozi
anautetea”amesema Doyo.
Doyo amedai kuwa chama chake kimchukulia hatua Bwana
Said Miraaj Abdulla,ni kutokana na kukiuka kanuni za chama kwa kitendo chake
cha kuongea na waandishi wa habari na kuongea mambo yanahusu chama hicho bila
ya kupata idhini ya chama hicho kama katiba inavyoelekeza.
Hata Hivyo, chama cha ADC kimemtaka Msajili wa vyama
vya siasa aache kubeba uongozi wanaodai kuwa sio wa kihalali kwa ni umesimamishwa kwa mujibu wa chama
hicho kifungu kidogo (1) h cha
Katiba ya chama hicho.
“Katiba inasema
endapo kwa sababu ya yoyote ile
chama kitakosa uongozi halali wa kikatiba au kitakuwa na mgogoro wa
uongozi na kukifanya kukosa uhalali wa kufanya shughuli zake,bodi ya wadhamini wa
chama kwa mujibu wa kifungo hichi itakuwa na mamlaka ya kamili ya kusimamia
shughuli za uendeshaji hadi hapo chama kitakapopata uongozi halali”amesema
Doyo.
Katika hatua nyengine chama hicho kimemtaka Rais
John Magufuli kuzingatia sheria ya nchi katika kubadilisha matumizi wa fedha
kama alivyofanya pale alipofuta sherehe za uhuru pamoja na muungano kwa
kuidhinisha pesa zile kwenda kwenye matumizi mengine.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni