MIRAJI AMLIPUA HAMADI RASHIDI...AMTAKA ATOKE HADHARANI
Hatimaye Mwenyekiti wa
Chama Cha Alliance for democratic Change(ADC)Saidi Miraaji,amemtaka Hamad
Rashid aache tabia ya kutumia vibaraka kuleta migogoro ndani ya chama badala
yake atoke hadharani wapambane kwa hoja.
Akizungumza na Waandishi
wa habari, Miraaji amesema sababu ya mgogoro wa chama ni Hamadi Rashidi,amekuwa
akifanya uvurugaji wa katiba na kanuni ya chama kwa kutumia vibaraka wake
“Nataka nimwambie Hamadi Rashidi atoke
hadharani apambane na mimi, kuendelea kuwa nyuma ya pazia huku akifadhili vikao
ambavyo vinalenga kunivua uenyekiti havitaweza kushinda kwa sababu chama
kinaongozwa kwa misingi ya katiba na Kananu”
Amesema hata ukiangalia
rekodi za Hamadi Rashid amekuwa ni mtu wa kufukuzwa kwa kila chama anachoingia
na hiyo inadhihirisha jinsi ambavyo alivyokuwa mvurugaji wa mambo.
Akizungumzia kuhusu
sakata la yeye kutimuliwa amesema yeye hana hana nia ya kung’ang’ania uongozi
lakini anachofanya ni kutaka kuonyesha umma kuwa kinachofanyika katika Chama
cha ADC si haki
Amesema kwa hali ilivyo
hata waende wapi hawataweza kushinda na kwamba atapambana kuona haki zake
zinapatikana, kwani anaamini kinachofanywa na viongozi waliopo ni kinyume cha
katiba ya chama
Nafahamu HAMAD RASHID anatamani leo kesho akamate
nafasi ya uenyekiti katika chama cha ADC lakini kwa jinsi anavyokwenda
anajiharibia, naona mwisho nwa mwanasiasa huyu unakaribia”Alisema Miraji.
Amesema kuwa tangu kumalizika kwa uchaguzi wa awali
visiwani Zanzibar HAMAD RASHID ambaye alikuwa mgombea wa chama hicho Visiwani
Zanzibar amekuwa akitoa matamko yanayokihusu chama bila kuwashirikisha viongozi
halali wa chama hicho likiwemo tamko la kukubali kushiriki katika uchaguzi wa
marudio wa Zanzibar tamko ambalo amesema halikuwa na Baraka za chama hicho.
MIRAAJ amewaeleza wanahabari kuwa yeye kama
mwenyekiti wa chama alimpokea HAMAD RASHID kama mwanachama wa kawaida na
baadae kukubali awe mlezi wa chama hicho kutokana na ukongwe wake katika siasa
za Tanzania lakini hawakumpa kazi ya usemaji wa chama kwani kwa mujibu wa
katiba ya chama hicho msemaji pekee wa chama hicho ni mwenyekiti.
Aidha Ameeleza kuwa kazi pekee ya mlezi wa chama ni
kuwashauri viongozi wakuu wa chama na sio kutoa maamuzi ya chama kama
aliyoyafanya ya kukubali kurejea uchaguzi wa Zanzibar bila ridhaa ya mwenyekiti
na vyombo husika vya chama,huku akimtaka aache kuivuruga katiba ya chama hicho.
Amesema kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho
baraza la wadhamini la chama halina nguvu yoyote kisheria ya kumuondoa
mwenyekiti madarakani kamali livyofanya hivyo yeye ataendelea kuwa mwenyekiti
wa chama hicho hadi pale ambapo itaamuliwana na sheria kuwa hafai kuwa
mwenyekiti huku akisema anajipanga kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa hapo
kesho kumweleza masikitiko yake ya kuzuiwa na watu ambao amewaita wahuni ndani
ya chama kurejea katika ofisi zake kama kawaida.
Hapo jana Naibu katibu mkuu wa chama hicho DOYO
HASSAN DOYO aliwaeleza wanahabari kuwa mwenyekiti huyo haruhusiwi kufika katika
eneo lolote la ofisi za chama hadi apate mwaliko maalum wa chama hicho tamko
ambalo mwenyekiti huyo SAID MIRAAJ amelikanusha na kusema kuwa limeandikwa
kihuni na wahuni wanaotaka kukivuruga chama na yeye hayupo tayari kuwavumilia.
Ameongeza kuwa tamko la chama hicho kwa wanahabari
la jana halina uhalali kwa kuwa limeandikwa kihuni bila saini ya
mwandikaji,bila jina la mwandikaji hivyo hakuna tamko la chama linalotoka
hivyo.
Mgogoro ndani ya chama hicho uliibuka mara tu baada
ya kumalizika kwa uchaguzi wa kwanza wa Zanzibar ambapo swala la uchaguzi wa
marudio liliwagawa viongozi hao huku ikionekana wazi kuwa mwenyekiti huyo
hakuwa tayari chama cha ADC kushiriki katika uchaguzi huo huku mgombea HAMAD
RASHID ambaye ameonekana kuwa na nguvu ndani ya chama hicho kushiriki katika
uchaguzi huo uliopelekea chama cha mapinduzi kuibuka na ushindi mnono.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni