CHADEMA YAFTUKA KWA RAIS MAGUFULI,YASEMA ANACHUKIA POMBE ZAIDI KULIKO UFISADI,SOMA HAPO KUJUA
HATUA ya Rais John Pombe Magufuli kumtimua kazi
Charles Kitwanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi imeibua maswali,” anaandika Pendo Omary.
Miongoni mwa maswali hayo ni
pamoja na kwamba, Rais Magufuli anachukia zaidi pombe kuliko ufisadi? Ni kwa
madai hukumu ya pombe imepewa kipaumbe zaidi juu ya mtuhumiwa zaidi ya harufu
ya ufisadi anaotuhumiwa nao.
Swali
hilo limehojiwa na Julius Mwita, Katibu Mkuu Baraza la Vijana (Bavicha) baada
ya kuzungumza na Mwanahalisi Online leo jijini Dar es Salaam. “Rais anachukia
pombe kuliko ufisadi?” amehoji.
Mwita
amedai kuwa, hatua ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Kitwanga ni kukwepa
mapendekezo yaliyotolewa na baraza hilo.
Mapendekezo
hayo ni kuhusu kumchukulia hatua Kitwanga ili kupisha uchunguzi wa mkataba tata
ulioingiwa kati ya Kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.
Katika
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jioni na Gerson Msigwa, Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu imeeleza kuwa “Rais Magufuli ametengua uteuzi
huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu
swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.”
Mwita
amesema “tulitaka Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga au Kitwanga
ajiuzulu mwenyewe ili kupisha uchunguzi wa mkataba tata baina ya Jeshi la
Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises.
“Hii
ingetoa uhuru kwa kamati ndogo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) kufuatilia suala hili kwa undani. Alichokifanya Magufuli ni
kuwaziba watu macho. Je, Magufuli anachukia zaidi ulevi kuliko ufisadi,”
amesema Mwita.
Mwita
amesema, uchunguzi utakaofanywa na kamati ndogo ya PAC unapaswa kuwekwa
hadharani na kujulikana kwa Watanzania wote ili waujadili.
“Baada
ya uchunguzi huo. Watu wote waliotajwa wanapaswa kuchukuliwa hatua zaidi. Rais
Magufuli aliahidi kufungua Mahakama ya Mafisadi, anapaswa kutimiza ahadi yake,”
amesema Mwita
Hakuna maoni
Chapisha Maoni