CCM YAMWANDALIA MIPANGO YA HOVYO MAALIM,SIRI ZAANZA KUFICHUKA,SOMA HAPO KUJUA
TAARIFA zimevuja. Wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wanatajwa kushinikiza Jeshi la Polisi kumkamata Maalim Seif Shariff
Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), anaandika Regina Mkonde.
Si Maalim Seif pekee, viongozi
wengine wa chama hicho wanaoundiwa mkakati wa kukamatwa ni pamoja na Mansoor
Yussuf Himid na Nohamed Ahmed Sultan kwa sababu za kisiasa.
Taarifa
hizi zinathibitishwa na Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar
ambaye amesema;
“Tunazo
taarifa kwamba, kuna wanasiasa wameliagiza Jeshi la Polisi kuandaa mashtaka kwa
ajili ya kumshitaki Maalim Seif Sharif Hamad kwamba alipokuwa Pemba alifanya
maandamano bila ya kibali wakati hakukuwa na maandamano yoyote.”
Mazrui
amesema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu
Zanzibar kwa mwaka 2015/2016 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
“Viongozi
hao wamepangiwa kukamatwa na kuletwa katika magereza ya Tanzania Bara kwa lengo
la kuwanyamazisha Wazanzibar ili wasipaze sauti zao kupinga utawala wa kidkteta
uliowekwa madarakani kwa nguvu za dola kinyume na matakwa ya kidemokrasia ya
wananchi wa Zanzibar,” amesema.
Akizungumzia
uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu Zanzibar 2015/2016
amesema, CUF inajiandaa kuchukua hatua kutokana na uharibifu uliofanywa na
Serikali ya CCM visiwani humo.
Mazrui
akimwakilisha Maalim Seif kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo amesema, nakala ya
ripoti hiyo pia watamkabidhi Rais John Magufuli kwa lengo la kujua kilichofanyika
na kinachofanyika Zanzibar.
“Baada
ya hatua ya leo ya uzinduzi wa taarifa hii, CUF kimejiandaa kuchukua hatua
ikiwemo ya kumuandikia rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Dk.
John Magufuli na kumkabidhi nakala ya taarifa hii ili ajue kinachofanyika
nchini na hasa akiwa Amiri Jeshi Mkuu,” amesema Mazrui.
Hatua
nyingine zitakazochukuliwa na CUF ni pamoja na kuiwasilisha taarifa hiyo pamoja
na vielelezo vyote katika Jumuiya, Taasisi za Mashirika ya Kimataifa
yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni ili kuchukua hatua zao.
“Pia
tutaiwasilisha taarifa pamoja na vielelezo vyote katika Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora hapa nchini ambayo hata katika mkutano wa Geneva
ilitambuliwa uwepo wake,” amesema na kuongeza.
“Na
katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar (ZLSC) pamoja na taasisi nyingine zinazoshughulikia masuala ya haki za
binadamu hapa nchini.”
Mazrui
amesema “ Hatua nyingine itakayofuatwa ni kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya
Tanzania dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP) kuhusiana na matendo yanayohusisha Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar.
Hatua
nyingine itakayochukuliwa ni CUF kukamilisha taratibu zitakazoiwezesha Mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya watu wenye dhama
mbalimbali ambao wamehusika kuchochea, kutoa au kusimamia maagizo
yaliyoepelekea makosa dhidi ya ubinadamu na makosa yaliyoilenga jamii ya watu
fulani
Habari hii kwanisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni