Zinazobamba

BREAKING NEWS,MEYA WA UKAWA KINONDONI ATUMBUA VIGOGO,WAKUTWA NA UFISADI WA KUTISHA,SOMA HAPO KUJUA



Meya wa Ukawa Manispaa ya Kinondoni,Bonifacce Jacob

BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wameridhia  hatua ya kumsimasha kazi Mwanasheria mkuu wa Manispaa hiyo Burton Mahenge pamoja na Mthamini wa Manispaa hiyo Eihard Chidaga kutokana  kuingia mikataba  ya utata ambayo imetia hasara Halmashauri hiyo bilioni zaidi ya Bilioni 7.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo

Akitangaza uamuzi huo mda huu  Jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob amesema uamuzi huo wa kuwasimamisha watendaji hao umetokana  na kikao cha madiwani kilichokaa jana, kimebaini Ubadhilifu kwenye mikataba iliyoingiwa na watendaji hao na kuisabisha Halmashauri hiyo kupata hasara.

Jaccob ametaja makosa hayo yaliyogundulika ni mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa ulioko jijini hapa ambao mradi huo umeikosesha halmashauri hiyo milioni 900 kwa mwaka lakini kutokana na mgogoro uliopo umeikosesha manispaa hiyo  shilling bilioni 4.5 kwa miaka mitano tangu mradi huo kuanza.

Amefafanua kuwa mradi huo ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili Na.277na 322 ambapo uwekezaji wake katika kiwanja 277 una nyumba  Na 322 Nyumba 68  lakini amedai kuwa mwekazaji huo wa nyumba hizo hajazilipia kodi.

Sanjari na hiyo,pia Jaccob ambaye ni Diwani wa Ubungo ametaja kosa jingine lilofanywa na Viongozi hao kuwa ni mogogoro wa upangaji wa nyumba za Magomeni Kata  umetokana na Mwansheria huyo kuingia Mkataba na wapangaji waliokuwepo katika eneo hilo ambapo mkataba huo unata kulipwa fedha ya milioni 1.080000  kwa mwaka wapangaji hao licha ya kuhama katika eneo hilo.

“Yaani huyo Mwanasheria ameingia mkataba Bogus treaty (mikataba ya kijinga) ambao kwa mwaka tunawalipa wapangaji hawa milioni moja kwa mwaka wakati wameshahama  katika eneo hili,kwahiyo kwa uzembe wa mkataba huo sasa hivi manispaa tunadaiwa  zaidi ya bilioni 3 kwa mwaka”amesema Jaccob,

Hata hivyo,Jaccob amesema baada ya Halmashauri hiyo kugoma kuwalipa fedha hizo,wapangaji hao wamekwenda kufungua Kesi Mahakamani na kutolewa hati ya Kukamatwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Aron Kagurumjuu,

Ameleza kuwa licha ya Hati hiyo kutolewa lakini Mwanasheria huyo alishindwa kumtaharifu Mkurugenzi wake wakati alikuwepo mahakamani jambo analosema linazidi ibua utata.
  
 MKATABA WA COCO BEACH.
Jaccob amesema Mahenge pia anahusika katika sakata la mkataba tata wa Coco beach kutoka na kitendo chake cha kuzembea mpaka serikali ikashindwa kesi mahakamani kwa hatua yake ya kutofika mahakamani wakati wa kesi hiyo ikisomwa, jambo analodai lilichangia mahakama  kuipa ushindi kampuni Q-Consult limited ambayo ni ya Mwenyekiti wa Klabu ya mpira ya Yanga,Yusufu Manji kuendelea na uwekezaj.

Licha kushindwa huko mahakamani pia Mahenge amepuuzia agizo la Rais John Magufuli lilotaka kesi hiyo ikatiwe rufaa lakini Mahenge tangu 2015 hukumu hiyo ilipotolewa hajakata rufaa mapaka sasa jambo linalotia mashaka uwenda naye anamslai ya Kampuni hiyo.

     MRADI WA UJENZI WA MADUKA YA MAKUMBUSHO (EASTERN CAPITAL LTD)

 Jaccob amedai kuwa madiwani hao wamebaini utata kwenye kituo hicho cha mabasi kilichopo makumbusho baada ya kugundulika halmashauri inapata mapato madogo ya milioni 4 kwa mwezi tofauti na mapato ya milioni 40  kwa mwezi kwenye kituo cha   awali cha Mwenge.

Amefafanu kuwa mkataba huo wa makumbusho  Halmashauri inapata asilimia 15 huku Mbia anapata asilimia 85 ya mkataba huo jambo linalolikosesha fedha Halmashauri  na kupelekea kuibua utata ya sababu ya kuhama kituo cha Mwenge chenye mapato makubwa.

Amedai kuwa katika eneo hilo pia  kuna jengo la gorofa huku jengo hilo  limeongezwa gorofa mbili ambazo amedai kuwa halmashauri hizo haipati fedha huku ujenzi wake ukiwa tofauti na mkataba unavyotaka kwani ulitaka kuwa na gorofa moja.

 Jaccob ametaja miradi mengine ya kiufisadi waliofanya watendaji hao ni Ujenzi wa Nyumba za Makazi  Hill ostarbei ambao amedai kuwa tangu mkataba huo usainiwa 2009 ,huku mkataba huo ukibadilisha matumizi ya awali ya mkataba huo bila halmashauri kutalifiwa  taarifa za ubadilishaji huo.

Nyingine ni ujenzi za Nyumba za Makazi kwanja Na.314 toure drive ambapo mkataba  huo unatekelezwa na ubia na kamapuni ya lake Oil limited  na mradio huo unaonekana kuingiwa mwaka 2019 ambao mda  haujafika,

Licha kudanganya mwaka pia mkataba huo unaoenkana umefanyiwa marekebisho bila kufuta idhini ya halmashauri na kuishabisha mradi kuchelewa kuanza na kupelekea kuiskosesha mapato serikal.

Vilevile,Jacob amesema baada ya kuwasimaisha watendaji hao,hautua inayofuata ni kuwachunguza na kuwapeleka mahakamani,huku akizitaka makampuni ya uwakili yalipo kwenye wilaya hiyo kujitokeza wakati viongozi hao watakapowapeleka mahakani ili watoe msaada wa kisheria.
A
Licha ya Kampuni hizo,pia Jacoob ameitaka Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kushirikana nao katika kuchunguza mikataba yote ambayo imeingiwa na watendaji hao kwani inaviashiria vya ufisadi.

Hakuna maoni