TIGO 4G SASA YAINGIA KANDA YA ZIWA...YAINGIA MIJI MITANO
Waandishi wa habari wakichukua taarifa |
Kampuni ya simu ya Tigo ambayo inaendesha maisha ya kidijitali Tanzania imetangaza
kuzinduliwa kwa huduma ya 4G LTE katika miji mingine mitano yakanda ya
ambayo ni Tabora, Musoma, Bukoba, Kigoma na Shinyanga
Kampuni
hiyo awali ilizindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam
mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye kuisambaza katika miji ya Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro,Moshi na Mwanza na
hivyo kuifanya kuwa
Ikiwa
inachukuliwa kuwa ni teknolojia nzuri na ya uhakika katika sekta ya mawasiliano ya simu duniani ya kupata intaneti, kasi yateknolojia ya 4G LTE ni takribani mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G na Tigo inaifanyia kazi kwa kina ili kuongeza ubora
wa huduma hiyo na mtandao wa 4G kutokana na matumizi ya wateja kuwa nayo
yanaongezeka kwa kasi kubwa.
Hivi
sasa Tigo ina timu inayofanya kazi saa zote kuimarisha na kukuza ubora wa teknolojia ya 4G. Matokeo yake ni kwamba mtandao wa 4G
umekuwa unategemewa kwenye miji ambamo upo (Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza).
Mtandao wa 4G LTE unatoa intaneti ya kasi ya
kurambaza (surf) na kupakua vitu, kufanya miito ya simu ya kuonana (Skype) isiyo na kikomo.
Kutokana na uzinduzi wa hivi karibuni wa video za bure kupitia
YouTube nyakati za usiku, mtandao wa 4G LTE unawawezesha wateja kwa kiwango kikubwa kupata uzoefu wa kutiririsha video zilizo na uangavu mkubwa. Aidha kutokana na ushirikiano
na Facebook mteja wetu wa 4G pia anaweza kufurahia kutiririsha video zilizomo kwenye mitandao maarufu ya kijamii duniani.
Pia, mteja akiwa na 4G LTE anaweza
kupakua mafaili makubwa (sinema, mafaili yanayohusiana na kazi) au vifaa na hali kadhalika kucheza michezo kwa njia ya mtandao.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez, alisema mpango wa kupanua teknolojia ya 4G
hadi kwenye maeneo yote ya nchi upo mbioni ambapo kampuni hiyo imejikita kwenye kuwapa wateja wake
huduma zenye ubora duniani ambazo zitawawezesha kufurahia mtindo wa
maisha ya kidijitali.
“Kupanua
mtandao wa 4G LTE nchi nnzima kwa mara nyingine kunaonesha sio tu Tigo kuongoza kwenye kutoa teknolojia na ubunifu wa kisasa
ndani ya soko bali pia kusisitizia kujituma kwetu katika kuongeza
fursa ya kufikia intaneti kwa Watanzania walio wengi kwa kadri
iwezekanavyo,’ alisema Gutierrez.
Kwa
mwaka huu 2016, Tigo itawekeza zaidi ya dola milioni 75 kwenye upanuzi wa mtandao na kuimarisha ubora wake kwa kukuza
maeneo ya teknolojia ya 4G na 3G, mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya sehemu za kutolea huduma kwa wateja nchi nzima. “Tukiwa kama kampuni tunatambua umuhimu wa wa ubora na ukaribu kwa wateja
wetu na tunafanya kazi ili kufikia malengo hayo katika siku za karibuni,” alisema Gutierrez.
“Hivi
sasa pia tuna programu ya kufanya mtandao kuwa wa kisasa ambao unajumuisha kuongeza uwezo wa 4G kwenye miji yote 12 ambako tuna mtandao wa 4G pamoja na kuongeza
mtandao wa 3G kufika maeneo yote nchini,” alisema Gutierrez na kuongeza kuwa wateja wa Tigo katika miji ya Mbeya, Mtwara na Lindi wajitayarishe kufurahia huduma ya Tigo 4G LTE itakayoanza kutolewa siku za hivi karibuni.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni